• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Mipangomiji
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu
      • Idara ya Maji na Usafi wa Mazingira
      • Idara ya Utumishi na Utawala
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Elimu Msingi

IDARA YA ELIMU YA MSINGI

Elimu ya Msingi imegawanyika katika hatua ama nyanja mbalimbali ikiwa ni Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi yenyewe kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na pia Elimu nje ya Mfumo Rasmi.

ELIMU YA AWALI 

Manispaa  ya Singida  ina jumla ya madarasa 56 ya awali yaliyosajiliwa.  Madarasa 47 ni ya shule  za serikali na  7 ni ya  shule zisizo za serikali.  Wanafunzi wote wa awali ni 7,329 Kati yao wavulana ni 3,450 Wasichana ni 3579. Wanafunzi wa awali wa shule za serikali  ni  6,744 kati yao wavulana ni 3,422 Wasichana ni  3,322. Wanafunzi wa awali wa shule  zisizo za serikali  ni  585 Kati yao wavulana ni 328 Wasichana ni  257.

ELIMU YA MSINGI

Manispaa ya Singida ina shule za msingi 54 zilizosajiliwa. Kati ya shule  hizo,  shule  47 ni za serikali  na 7 ni shule zisizo za serikali. Wanafunzi wote wa shule za msingi ni 34,002 wakiwemo  wavulana  16,483  na wasichana 17,519. Wanafunzi wa shule za msingi  za serikali ni 32,444 wakiwemo  wavulana  15,689  na wasichana 16755 . Idadi ya wanafunzi katika shule zisizo za serikali  ni  1,558, wavulana 794  na wasichana764. Idadi ya walimu wenye ajira ya kudumu wanaofundisha  shule za msingi  za serikali ni 714 wa kiume 196 na wa kike 518 na walimu wa shule za zisizo za serikali ni 86 wa kiume 86 Na wa kike 37

ELIMU MAALUM

Manispaa ina shule nne zinazitoa  huduma ya elimu maalum  kwa  wanafunzi wenye mahitaji maalum. Shule hizo ni Ipembe kwa ajili ya wanafunzi wenye uoni hafifu na ulemavu wa akili, Unyankindi  kwa ajili wanafunzi wenye ulemavu wa akili ,  Somoku kwa ajili ya ulemavu wa akili  na Tumaini Viziwi kwa ajili ulemavu wa  kusikia.  Shule hizi zina jumla ya  wanafunzi 155 wenye mahitaji maalum, wavulana 77 na wasichana78.

UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI DARASA KWANZA  

Kwa mujibu wa kifungu cha 35 cha sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na marekebisho yake ya mwaka 1995 watoto wote wenye umri wa kuingia shule ya msingi wanatakiwa kuandikishwa darasa la kwanza. Hali ya uandikishaji wanafunzi darasa la kwanza kuanzia mwaka 2011 imeoneshwa hapa chini.

Jedwali Na. 1: Hali ya uandikishaji wanafunzi darasa la kwanza kuanzia mwaka 2011 hadi 2017


MWAKA

LENGO

WALIOANDIKISHWA

%

Wav.

Was.

JML

Wav.

Was.

JML

2011

2170

2217

4387

2278

2284

4562

104

2012

2167

2179

4346

2119

2138

4257

98

2013

2277

2429

4706

2257

2409

4666

98

2014

2012

2133

4135

1901

1916

3817

92.3

2015

2016

1507

3523

2030

1995

4025

114.2

2016

2280

2364

4644

3204

3207

6411

138

2017

3614

3590

7204

3544

3519

7064

98


Chanzo  Halmashauri ya Manispaa ya Singida

MAENDELEO YA TAALUMA

Maendeleo ya taaluma  katika Manisipaa ya Singida yamekuwa yakiongezeka  kila mwaka  hususan kwa kipimo cha mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kupata wanafuzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari kama jedwali hapa chini linavyoonesha.

Jedwali Na. 2: Hali Halisi ya Maendeleo ya Taaluma


MWAKA

WALIOFANYA

WALIOFAULU

%

WALIOCHAGULIWA

%

2011
2340
2412
4752
1569
1474
3043
64.03
1569
1474
3043
100
2012
1724
2011
3735
1049
1025
2074
55.5
2049
1025
2074
100
2013
1529
1757
3286
978
965
1943
59.1
978
965
1943
100
2014
1154
1480
2364
764
957
1721
65.3
764
957
1721
100
2015
1234
1628
2862
875
1083
1958
68.41
875
1083
1958
100
2016
1311
1608
2919
948
1178
2126
72.83
948
1178
2126
100


Chanzo  Halmashauri ya Manispaa ya Singida

HALI YA MIUNDOMBINU 

Katika utoaji wa elimu ya msingi  iko miundombinu ya aina mbalimbali inayotumika. Baadhi ya miundombinu hiyo iliyo muhimu zaidi  ni pamoja na vyumba vya madasrasa, nyumba za walimu, ofisi za walimu wakuu, ofisi za walimu,maktaba, mwatundu ya vyoo, stoo na madawati.

Jedwali Na. 3: Hali ya Miundombinu.


Na.
AINA YA MIUNDOMBINU

MAHITAJI

ILIYOPO

UPUNGUFU

1
Vyumba vya madarasa

1,021

479

542

2
Nyumba za walimu

849

114

735

3
Ofisi za walimu wakuu

60

58

2

4
Ofisi za walimu

132

64

68

5
Maktaba

56

4

52

6
Matundu ya vyoo

1,666

937

729

7
Stoo

77

27

50

8
MADAWATI

13,774

12,173

*2,046


Chanzo  Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • *Upungufu huo wa madawati ni kama haupo na hauna athari kwa sababu madarasa ya  awali  wanasoma nusu siku kwa kuhudhuria awamu mbili kwa siku (double session) yaani asubuhi na mchana. Hivyo madawati yayotumika awamu ya asubuhi hutumika pi na wale wanafunzi wanaohudhuria awamu ya mchana. 

ELIMU NJE YA MFUMO RASMI

Elimu nje ya mfumo rasmi inajumuisha Elimu ya watu wazima, Mpango wa Elimu ya Msingi Kwa Walioikosa (MEMKWA), Mpango wa Elimu  ya Sekondari Kwa  Walioikosa (MESKWA) na elimu ya kujiendeleza.

MEMKWA

Wanafunzi wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa  inajumuisha makundirika mawili ambayo ni kundirika la kwanza na kundirika la pili hali ya MEMKWA  katika Manispaa ya Singida inafafanuliwa katika jedwali hapa chini.

Jedwali Na 4: HALI YA MEMKWA 


NA
KITUO

KUNDI RIKA LA KWANZA

KUNDI RIKA LA KWANZA

JUMLA

ME
KE
JML
ME
KE
JML
ME
KE
JML
1
MINGA

2

0

2

0

0

0

2

0

2

2
KINDAI

13

9

22

16

10

16

29

19

38

3
UNYAKUMI

5

1

6

3

2

5

8

3

11

4
SOMOKU

7

4

11

8

4

12

15

8

23

5
UKOMBOZI

22

29

51

0

0

0

22

29

51

6
UHAMAKA

7

8

15

0

0

0

7

8

15

7
MWANKOKO

31

21

52

0

0

0

31

21

52

8
SINGIDANI

10

8

18

2

0

2

12

8

20

 
JUMLA

97

80

177

29

16

35

126

96

212


Chanzo  Halmashauri ya Manispaa ya Singida

MPANGO WA ELIMU YA SEKONDARI KWA WALIOIKOSA (MESKWA)

Mpango wa Elimu  ya Sekondari Kwa  Walioikosa (MESKWA) unajumuisha   hatua ya kwanza  ambao ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mtihani wa maarifa (qualifying test) na hatua  ya pili  ambayo inahusisha  wanafunzi  wanaojiandaa kufanya mtihani wa kidato cha nne. Mpango huu unatekelezwa na vituo sita vya serikali na visivyo vya serikali kwa vilivyoorodheshwa  hapa chini kwenye jedwali hapa chini.

  

Jedwali  Na. 5: MPANGO WA ELIMU YA SEKONDARI KWA WALIOIKOSA  (MESKWA)


 NA

JINA LA TAASISI

HATUA YA I (qualifying test)

HATUA YA II (O LEVEL)

JUMLA

KE

ME

JML

KE

ME

JML

KE

ME

JML

1

SINGIDA FDC

6

4

10

10

11

21

16

15

31

2

TR CENTERS

22

14

36

47

26

73

69

40

109

3

TAASISI YA EWW

6

3

9

2

6

8

8

9

17

4

BRAC

0

0

0

44

0

44

44

0

44

5

SINGIDA LEARNING  OPEN  SCHOOL

5

6

11

20

5

25

25

11

36

6

SINGIDA YOUTH CENTRE

19

12

31

25

17

42

44

29

73

 

JUMLA

58

39

97

148

65

213

206

104

310


Chanzo  Halmashauri ya Manispaa ya Singida

Pamoja na kuwepo kwa mafanikio kama ilivyoelezwa hapo juu Manipaa ya Singida inakabiliwa pia na changamoto mbalimbali na baadhi ya changamoto hizo zimewekewa mikakati ka inavyoonekana hapo chini.


NA
CHANGAMOTO
MIKAKATI
1
Upungufu wa majengo ya shule ikiwa ni pamoja na vyumba 542 vya madarasa, nyumba 735 za walimu na miundombinu mbalimbali inayopunguza ufanisi.
Halmashauri imetenga fedha kwenye bajeti ya 2017/18 kwa ajili ya kupungaza uhaba wa miundombinu. Halmashauri inaendelea kushirikisha wadau mbalimbali ili kusaidia kupunguza  uhaba wa miundombinu mbalimbali inayohitajika
2
Upungufu wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia unaotokana na ufinyu wa fedha za kununulia vifaa hivyo.
Kuhamasisha jamii na wadau mbalimbali wa elimu kusaidia kupata vifaa hivyo.
Kupeleka takwimu za mahitaji ya vifaa hivyo serikalini kupitia ripoti zetu ili vipatikane.
3
Wazazi kutosimamia na kutofuatilia maendeleo ya watoto wao katika masomo pamoja na kutoa ushirikiano mdogo kwa walimu hali  inayosababisha utoro
Kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto wao.
Baadhi ya wazazi wenye watoto watoro kufikishwa kwenye Mabaraza ya Kata na hata mahakamani.


Matangazo

  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021 - HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA December 23, 2020
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 December 17, 2018
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2018 KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA January 24, 2019
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MKUU wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema Nchimbi (aliyefunga kilemba kichwani) akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa vitanda na madawati kwa uongozi wa shule ya sekondari ya New Kiomboi.

    June 21, 2020
  • DKT. REHEMA NCHIMBI, AZINDUA RASMI HUDUMA ZA CHF ILIYOBORESHWA, MKOANI SINGIDA

    April 11, 2019
  • MKOA WA SINGIDA WAANZA KUCHUKUA HATUA KATIKA KUKABILIANA NA HALI DUNI YA LISHE KWA WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO

    November 14, 2018
  • DIWANI WA MANISPAA YA SINGIDA AFARIKI DUNIA

    May 22, 2018
  • Tazama Zote

Video

Waziri Jafo atoa maagizo mazito kwa ma-RAS, ma-DED, Wakuu wa idara na maasifa mawasiliano serikalini
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.