• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DKT. REHEMA NCHIMBI, AZINDUA RASMI HUDUMA ZA CHF ILIYOBORESHWA, MKOANI SINGIDA

Posted on: April 11th, 2019


Tarehe Ya Kuwekwa: April 11th, 2019

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi  Aprili 10, 2019 amezindua rasmi huduma za Afya za CHF iliyoboreshwa katika mkoa wa Singida ambapo amewataka wananchi wa mkoa wa Singida kujitokeza kwa wingi ili kujisajili katika huduma za BIMA na CHF iliyoboreshwa ili kuwa na uhakika wa tiba kwa familia zao kwa mwaka mzima ndani ya mkoa katika hospitali zote zilizounganishwa na mfumo wa CHF uliyoboreshwa.

Dkt. Nchimbi akizungumza na wananchi hao amesema, kutokujali na kuzingatia afya, na kufanya makusudi ya kutokujihusisha na miundombinu na mifumo ambayo imeelekezwa na kuandaliwa na Serikali ya kumsaidia kila mwananchi kuwa na uhakika wa afya bora ni kosa la kijinai.

 “Tunasisitiza kwamba kila mkazi wa mkoa wa Singida, ahakikishe anajiunga na mfuko huu ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu hata wakati hana fedha”

“Kuna watu wenye fikra potofu eti hawawezi kujiunga na bima ya afya kabla ya kuugua. Huo ni uchuro mkubwa”.


“Ugonjwa hauna tabia ya kutoa taarifa kuwa tarehe fulani utamkumba mtu fulani. Unakuja ghafla bila matarajio ya mhusika. Mhusika anakuwa hana hela wala mjomba wa kumsaidia, hii ni hatari kwa usalama wa mtu huyo”. amesema Dkt. Nchimbi Aidha, Mkuu huyo wa mkoa wa Singida, amewahimiza wananchi hao kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kuepusha miili yao kuwa nyumba ya milolongo ya magonjwa mbalimbali yasiyoisha.

Amesema, binadamu mwenye nguvu ya kufanya kazi na akawa hafanyi kazi, mwili wa mtu huyo  hudhoofika  kwa kasi na kuruhusu kirahisi magonjwa ya kila aina kumuingia.

“Wavivu wa aina hii wanaoruhusu kwa makusudi maradhi kuwaingia, BIMA iliyoboreshwa sio rafiki yao. Kufanya kazi kwa bidii ni  kinga tosha ya mwili. Asiyefanya kazi kwa bidii huyo anaruhusu magonjwa kumwingia kirahisi”, Dkt. Nchimbi

Akifafanua zaidi kuhusu bima ya afya iliyoboreshwa amesema, ni kinga tosha inayomlinda mwanachama na familia yake ya mke/mme mmoja na watoto wanne walio na umri wa chini ya miaka 18.

Kwa upande wake mwakilishi wa Meneja wa CHF Taifa, Slivery Mgonza, amesema bima hiyo imeboreshwa pamoja na mambo mengine, imepanua maeneo ya kutoa huduma. Kwa sasa mwanachama atakuwa na fursa ya kutibiwa sehemu yoyote ndani ya mkoa tofauti na zamani.

Amesema, usajili wake kwa sasa umekuwa rahisi, mambo ya kalete picha sasa hayapo. Kila kitu kinapatikana kwenye vituo vya usajili.

Naye, Mganga mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Victoria Ludovick amesema kuanzia Januari hadi Desemba mwaka 2018, idadi ya walengwa  wa CHF walitambuliwa, kati yao 54,569 walifanikiwa kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii. 

Akisisitiza zaidi amesema, jumla ya shilingi 502,825,000, za mfuko wa CHF zilikuwasanywa kutoka halmashauri zote saba. Fedha za tele kwa tele zilizoombwa na halmashauri zote ni shilingi 347,889,000. Kati ya hizo, shilingi 20,330,000 tu, zililipwa kwa halmashauri ya Ikungi.

Wakati huo huo, fundi ujenzi manispaa ya Singida, Hassan Ikingu ambaye alijiunga na mfuko huo jana, amesema mfuko huo wa bima pamoja na faida zake nyingi, unasaidia mno kupunguza gharama kubwa za sasa za matibabu. 

“Sasa hivi kwa sisi wananchi wenye kipato cha chini, si rahisi kumudu gharama za matibabu zinazotozwa na vituo vya kutolea huduma za afya. lakini ukiwa na bima ya afya ya jamii, hata kama huna fedha unauhakika wa kupata matibabu ya gharama yoyote”, amesema Ikingu.


MATUKIO KATIKA PICHA 

 Huduma za usajili wa BIMA iliyoboreshwa zikiendelea kutolewa kwa wananchi katika uwanja wa zamani wa stand ya mabasi katika Manispaa ya Singida, wakati wa kilele cha uzinduzi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) ulioboreshwa, mkoani Singida.

 Kikundi cha ngoma cha mbalamwezi kikitoa burudani wakati wa kilele cha uzinduzi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) ulioboreshwa, mkoani Singida.  

  Mganga mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Victoria Ludovick akizungumza wakati wa kilele cha uzinduzi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) ulioboreshwa, mkoani Singida.  

  Mwakilishi wa Meneja wa CHF Taifa, Slivery Mgonza, akizungumza wakati wa kilele cha uzinduzi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) ulioboreshwa, mkoani Singida. 

  Katibu Tawala mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akizungumza wakati wa kilele cha uzinduzi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) ulioboreshwa, mkoani Singida.

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye kisemeo) akihamasisha zoezi la uchangiaji wa huduma za CHF iliyoboreshwa kwa ajili ya kuwapatia wananchi wasio na uwezo wa kuchangia, wakati wa kilele cha uzinduzi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) ulioboreshwa, mkoani Singida.

 Katibu Tawala mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi (wa pili kulia) akichangia huduma ya CHF iliyoboreshwa kwa ajili ya mwananchi mmoja (aliyebeba mtoto) ili aweze kupatiwa kadi ya huduma ya afya ya CHF iliyoboreshwa, wakati wa kilele cha uzinduzi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) ulioboreshwa, mkoani Singida.


 Mganga mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Victoria Ludovick akichangia huduma ya CHF iliyoboreshwa kwa ajili ya mwananchi mmoja (mama mjane, wa kwanza kulia) ili aweze kupatiwa kadi ya huduma ya afya ya CHF iliyoboreshwa, wakati wa kilele cha uzinduzi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) ulioboreshwa, mkoani Singida.


 Mwakilishi wa shirika la World Vision mkoani Singida akipongezwa mara baada ya kuchangia kaya kadhaa za halmashauri mbalimbali za mkoa wa Singida ili aweze kupatiwa kadi ya huduma ya afya ya CHF iliyoboreshwa, wakati wa kilele cha uzinduzi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) ulioboreshwa, mkoani Singida.


 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza, wakati wa kilele cha uzinduzi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) ulioboreshwa, mkoani Singida.


 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mara baada ya kubonyeza king'ola cha uzinduzi rasmi wa CHF iliyoboreshwa mkoani Singida wakati wa kilele cha uzinduzi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) ulioboreshwa, mkoani Singida.


 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akikabidhi kadi za huduma ya afya za CHF iliyoboreshwa, wakati wa kilele cha uzinduzi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) ulioboreshwa, mkoani Singida.


 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na watoto pamoja na mwakilishi wa wazazi waliopatiwa kadi za huduma za CHF iliyoboreshwa, wakati wa kilele cha uzinduzi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) ulioboreshwa, mkoani Singida.


 Sehemu ya wananchi mbalimbali waliojitokeza kushuhudia kilele cha uzinduzi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) ulioboreshwa, mkoani Singida.


 Sehemu ya meza kuu 

   

 

 


Matangazo

  • NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA SINGIDA June 03, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • VIKUNDI 55 VYAPATIWA MAFUNZO KABLA YA KUPOKEA MIKOPO YA 10%

    June 29, 2025
  • SINGIDA MANISPAA YAANZA KUTOA ELIMU YA UCHAGUZI MKUU KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • USAFI WA NGUVU KUELEKEA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA WAFIKIA ASILIMIA 80

    June 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.