• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

AFRIKA YAASWA KUBORESHA MIFUMO YA TAKWIMU KWA MIPANGO MADHUBUTI YA MAENDELEO

Posted on: November 29th, 2022

TANZANIA imeyataka Mataifa ya Afrika, kuboresha taratibu na mifumo ya ofisi za Takwimu, ili ziwe bora na zenye tija katika nyanja mbalimbali, ikiwemo sekta ya Kilimo, lishe na usalama wa chakula, kwa nchi husika.

Hayo yamebainishwa leo Novemba 29, mkoani Singida, na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, aliyewakilishwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde, kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika, yaliyofanyika kitaifa Mkoani Singida.

Amesema kuwa, maboresho ya mifumo ya Takwimu, iwapo yataboreshwa kwa kila nchi katika  Bara hili, itarahisisha katika utekelezaji wa mipango ya kimaendeleo na kutoa matokeo chanya kwa jamii.

“Kauli mbiu hii, inazitaka nchi za Afrika, ziboreshe mifumo ya Kitakwimu kuwa bora, iweze kuzalisha Takwimu za kilimo na kisasa, ili kuboresha sera za Kilimo, zitakazoleta Uhimilivu wa Kilimo, lishe na usalama wa chakula,” amesema Dk. Mwigulu kupitia Naibu Waziri wa Kilimo, Mavunde.

Naye Kamishna wa Sensa (2022), Anna Makinda, amesema Sensa ya mwaka huu iliyofanyika mwezi Oktoba, itawezesha Serikali kuandaa Mipango yake,ya Maendeleo, kutokana na idadi ya watu waliopo.

“Tufanye suala la Sensa liwe kweli, tuache kuamua tu mambo kwa mabavu, …. mtu mwenye mabavu fulani kupeleka kitu mahali, na kumbe wengine wanahangaika,” amesema Makinda.

Kuhusu vijana, Kamishna wa Sensa, amelitaka kundi hilo, kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa, kwa lengo la kujipatia maendeleo binafsi na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba amewakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika mkoa wa Singida kutokana na uwepo wa miundombinu bora na fursa nyingi za uwekezaji katika sekta za kilimo, viwanda, utalii na nishati.

Aidha amesema Mkoa wa Singida unatekeleza mipango yake kwa kupitia takwimu za za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ambapo mkoa unawatu wapatao 2,008,058 wakiwemo wanawake 1,012,355na wanaume 995,703.

 

Kauli Mbiu ya siku ya Takwimu Mwaka huu ni, ‘Kuimarisha mifumo ya Kitakwimu, kwa kutumia njia za kisasa katika uzalishaji na matumizi ya Takwimu za Kilimo ili kuboresha Sera kwa lengo la kuimarisha uhimilivu katika Kilimo, lishe na usalama wa chakula Afrika’.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.