• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SINGIDA LAPITISHA TAARIFA YA HESABU KWA MWAKA WA FEDHA UNAOISHIA JUNI 30, 2022

Posted on: September 29th, 2022

BARAZA la madiwani, Manispaa ya Singida limeridhia taarifa ya hesabu za halmashauri kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2021/22 katika Mkutano wake maalumu, uliofanyika leo tarehe 29 Septemba, 2022 kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Mwenge.

Taarifa hiyo ya hesabu za halmashauri ya Manispaa imejumuisha mizania ya hesabu ( |Statement of Financial Position) Taarifa ya Ufanisi ( Statement of financial performance), Taarifa ya mabadiliko ya mali halisi ( Statement in change of net asset), Mtiririko wa fedha ( Cash flow statement) na taarifa ya mlinganisho kati ya bajeti na uhalisia ( statement of comparison budget vs actal)

Akiongea baada ya kupitishwa kwa tarifa  hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Maulid Kiaratu amefafanua kuwa baraza la madiwani kupitia na kuridhia taarifa ya hesabu za halmashauri ni takwa la kiseria  na kikanuni na kwamba uandaaji wa taarifa hiyo umekuwa shirikishi baina ya wataalamu kutoka ngazi ya Manispaa, OR-TAMISEMI na Serikali kuu.

“ sina shaka na uandaaji wa taarifa hii kwani iko vizuri lakini napenda kuwapa ushauri wa kuipitia tena kabla ya kuikabidhi kwa CAG” aliasa Meya.

Ametaja kipengele cha utekelezaji wa miradi kuwa kimekuwa chini kutokana na miradi iliyopokea fedha kushindwa kukamilika kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali na kutoa agizo kwa watalaamu kuhakikisha wanasimamia vyema fedha za miradi ili iweze kutekelezwa  kwa wakati na hivyo kuondoa uwezekano wa mapungufu wakati wa ufungaji wa hesabu lakini pia kuondoa hoja za ukaguzi.

Kuhusu suala la usimamizi wa sheria ndogo, Mhe Kiaratu amewata watendaji wa kata kusimamia vyema sheria ndogo hasa katika suala la ukusanyaji mapato  ili kuongeza makusanyo ya ndani na kufikia malengo kusudiwa.

Pamoja na hayo, amesisitiza kuhusu upimaji wa maeneo ya taasisi ili kuongeza thamani ya mali za halmashauri pia kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Mjini, Shaban Kalaghe  amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na wataalamu ya kuandaa taarifa ya hesabu za Halmashauri kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2022 na kusema kuwa taarifa hiyo imekidhi viwango.

Kalaghe aliwapongeza wajumbe wa baraza la madiwani na wataalamu  kwa kupitisha eneo lililopendekezwa kwa ujenzi wa ofisi mpya za Manispaa lililopo Mtaa wa Karakana Kata ya Misuna na kusema kuwa wamefanya maamuzi sahihi katika kuupanua mji.

Hata hivyo Kalaghe amesisitiza umuhimu wa kutumia rasilimali halisi     (Asset) ili kuleta maendeleo ya Manispaa kwa kuweka vitegauchumi ambavyo vitaongeza mapato ya ndani.

Naye Mkuu wa Wilaya Singida Mhandisi Paskasi Muragili amewataka wataalamu na waheshimiwa madiwani kusimamia fedha za miradi hasa za ujenzi wa madarasa ambazo tayari zimetolewa na serikali.

Muragili amesema kuwa kukamilika mapema kwa vyumba vya madarasa kutawezesha wanafunzi  watakao jiunga na elimu ya sekondari na msingi hapo mwakani kuwa na mazingira mazuri ya kujifunzia.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.