• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BASHE: WAKULIMA WAPEWE MREJESHO WA TAFITI ZA KILIMO

Posted on: October 5th, 2022

Serikali Imeagiza matokeo ya tafiti za kilimo zinazofanywa na wataalamu, zirejeshwe kwa wakulima kwa ajili ya kuwawezesha wakulima, kutekeleza kilimo cha kisanyansi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa kilimo Hussen Bashe wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo kwa mwaka 2022/2023, katika mkoa Singida, Manispaa ya Singida.

Bashe amesema kuwa, wakulima wanachohitaji hivi sasa ni kuendesha kilimo chenye tija, ambacho kinawezekana kwa kupitia tafiti mbalimbali zitakazowezesha upatikanaji wa mbegu bora, matumizi ya pembejeo  na uwekezaji wa Miundombinu ya kilimo.

Amesema katika kuhakikisha wakulima wanapata huduma hizi, Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 80, kuwezesha kilimo cha ki-sayansi, kutoka Bilioni 16 zilizotengwa katika bajeti iliyopita (2021/2022).

“ Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kufanya mapinduzi makubwa ya kilimo…mkulima asipopata taarifa za kitafiti  na kuzifanyia kazi, ni sawa na kazi bure”, amesema Bashe

Akielezea matumizi ya fedha hizo Waziri Bashe amesema kuwa, zitatumika kufanya tafiti mbalimbali za mbegu, kutengeneza mpango mkubwa na wa muda mrefu wa kilimo, kufanya uwekezaji katika Miundombinu ya umwagiliaji, na kubanisha kuwa mabwawa 13 yatajengwa katika mikoa 7.

Aidha Waziri Bashe amefafanua kuwa, fedha zingine zitawajengea uwezo maafisa ugani kielimu, kuwapatia vitendea kazi, ambavyo ni vishikwambi vitakavyounganishwa na mfumo wa usimamizi  wa shughuli za ugani na kupatiwa vifaa vya kupima ubora wa udongo kwa ajili ya kilimo.

Amesema Wizara yake tayari imepokea mahitaji ya mbegu bora za alizeti zinzohitajika katika mkoa wa Singida, mahitaji yakiwa ni jumla ya tani 500 zitakazosambazwa katika halmashauri saba za mkoa huo, kati ya tani 2,900 zinazotarajiwa kuzalishwa  kukidhi mahitaji ya nchi nzima.

Mkoa wa Singida ni kati ya mikoa wa kimkakati kwa zao la Alizeti na tayari tani 19 zimekabidhiwa kwa Halmashauri mbili leo na Waziri wa kilimo, ikiwemo Manispaa ya Singida iliyopata mgawo wa tani 4 na Halmashauri ya Wilaya ya Singida tani 15.

Awali mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba, alisema kuwa ili kuondoa umaskini kwa watanzania, uwekezaji katika kilimo ni muhimu, na akatumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwekeza katika kilimo cha ki-sayansi kinachozingatia tafiti na umwagiliaji.

Serukamba alimhakikishia Waziri wa kilimo kwamba Mkoa huo, umejipanga vema kuongeza maeneo ya kilimo, na ameagiza AMCOS kuhakikisha wanatoa elimu sahihi kwa wakulima kuhakikisha wanachama wao wanajisajili kwenye daftari la wakulima na baadae kupatiwa mbegu na mbolea za ruzuku.

Serikali imetoa nafuu kwa wakulima katika ununuzi wa mbegu bora na mbolea, ambapo wakulima watanunua mbegu hizo, kilo moja kwa Shilingi 5,000 na Mfuko wa mbolea kwa Shilingi 70,000.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Alhaji Juma Kilimba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa kuwekeza fedha nyingi katika bajeti ya wizara ya kilimo msimu huu 2022/2023, ili kuwezesha kilimo cha kimkakati na kisayansi chenye Tija.

Amesema Mkoa wa Singida ni mkoa wa wakulima hivyo wakulima hawanabudi kulima kitaalamu zaidi, kwani bila kilimo mkoa hauwezi kusonga mbele.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.