• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

CHONGOLO: TOENI USHAURI NA MAONI KUHUSU UWEKEZAJI WA BANDARI, UTAKAOBORESHA NA KULETA TIJA KWA TAIFA

Posted on: July 24th, 2023

Watanzania wametakiwa kutoa ushauri na maoni au  mapendekezo yanayohusu uwekezaji unaofanywa kwenye bandari ya Dar es Salaam, ambao utachukuliwa na kufanyiwa kazi, kwa ajili ya kulinufaisha taifa.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema hayo jana tarehe 23 Julai, 2023, kwenye Mkutano wa hadhara, wa kanda ya kati, uliohusisha mikoa mitatu ya, Singida Dodoma na Tabora.

Mkutano huo, ulilenga zaidi katika kuwajengea wananchi uelewa wa kutosha, kuhusiana na  manufaa ya uwekezaji, katika sehemu ya bandari ya Dar es Salaam, utakaotekelezwa na mwekezaji DP World ya Dubai, kutoka nchini Saudi Arabia.

Chongolo amesema, serikali kupitia wataalamu wake imefanya uchambuzi na mapitio ya kina na kujiridhisha pasipo shaka kwamba, uwekezaji huo, utaleta tija na kunufaisha Watanzania.

Aidha Katibu huyo amesema, uwekezaji huo ni utekelezaji wa ilani ya CCM ibara Na 22 na 59, zilizofafanua zaidi umuhimu wa kujenga mazingira ya kushirikisha sekta binafsi, katika kuboresha utendaji kazi, na bandari ya Dar es Salaam ikiwa sehemu husika.

Hata hivyo kupitia mkutano huo, Chongolo ametoa tahadhari dhidi ya kauli za kejeli zinazotolewa na baadhi ya watu, wanaopinga shughuli za uwekezaji nchini, na kuonya kuwa, Tanzania hivi sasa inahitaji uwekezaji zaidi, ili  kustawisha uchumi wake.

“Vita ya uchumi, ni suala nyeti na linalohitaji tahadhari kubwa, ili kuepuka kupoteza uwekezaji wa lazima hapa nchini,” amesisitiza Chongolo

Katika hatua ingine Chongolo amepongeza utekelezaji wa miradi ya maendeleo, unaofanywa na serikali Mkoani Singida, na kubainisha kuwa, mabadiliko yanayoonekana sasa kwa sekta ya elimu, afya, maji na barabara, ni matokeo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema mkataba wa bandari umezingatia sheria zote za uwekezaji  wa bandari ya Dar es Salaam na kwamba suala la mipaka na ulinzi, litabaki kuwa jukumu la msingi la serikali.

Kuhusu faida za uwekezaji huo Prof. Kitila amesema pato la nchi litokanalo na bandari litaongezeka kutoka Tsh. Trilioni 7.76 kwa sasa, hadi kufikia Tsh. Trilioni 26 mwaka 2032/2033, hivyo kuwezesha miradi mikubwa ya ndani ya nchi kutekelezwa kwa wakati, na midogo nayo kwa maendeleo na ustawi wa Watanzania.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuupatia Mkoa wa Singida fedha za kutosha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo, huku kwa kipindi cha miaka miwili, mkoa wa Singida umepokea fedha zaidi Tshs. Bilioni 437 sawa na asilimia 252 katika kipindi hicho.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.