• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DC GONDWE AWAPONGEZA, WAFANYABIASHARA,AHAIDI SERIKALI ITAENDELEA KUTOA ELIMU YA MANUNUZI, ULIPAJI KODI

Posted on: February 12th, 2025





Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Godwin Gondwe, amewapongeza wafanyabiashara wa wilaya hiyo kwa juhudi zao katika kuendeleza biashara na kuchangia mafanikio ya mkoa, huku akiwataka wataalam kutoka Serikalini kuendelea kutoa elimu kuhusu mfumo wa manunuzi wa NeST na ulipaji wa kodi.



Mhe. Gondwe ametoa pongezi hizo leo Februari  12, 2025 wakati wa ufunguzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Singida, ambalo limefanyika katika Ukumbi wa Jalmin Hoteli, Manispaa ya Singida. 



Baraza hilo linalojumuisha wafanyabiashara, taasisi za serikali, sekta binafsi, pamoja na wataalam kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Singida na Wilaya ya Singida, lengo lake ni kuboresha mazingira ya biashara na kujenga ushirikiano mzuri kati ya wafanyabiashara na Serikali.



Akiwahutubia washiriki wa Baraza hilo, Mhe. Gondwe alisema kuwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Singida wamekuwa chachu ya mafanikio ya mkoa huo, na kwamba wanastahili kupongezwa kwa juhudi zao katika kuendesha biashara na kushirikiana na Serikali katika ukusanyaji wa mapato. Alisisitiza kuwa wafanyabiashara wamekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa wilaya hiyo na mkoa kwa ujumla.



"Nawapongeza wafanyabiashara wa Wilaya ya Singida kwa namna wanavyofanya kazi nzuri na namna ambavyo wamekuwa wakishirikiana na Serikali katika ukusanyaji wa mapato," alisema Mhe. Gondwe.



Pamoja na pongezi hizo, Mhe. Gondwe aliongeza kuwa Serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanapata mazingira bora ya kufanya biashara. Alizitaka idara na vitengo husika kutoa elimu ya kutosha kwa wafanyabiashara kuhusu matumizi ya mfumo wa manunuzi wa NeST (National e-Procurement System) na ulipaji wa kodi, ili kuongeza ufanisi katika biashara na michakato ya manunuzi serikalini.



“Tunawaomba wataalam kutoka Serikalini kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu mfumo huu wa NeST pamoja na namna ya kulipa kodi, kwani elimu hii itawawezesha wafanyabiashara kufanyakazi zao kwa ufanisi na kwa kuzingatia sheria,” alisisitiza Mhe. Gondwe.



Baraza hilo la biashara limekuwa  likitoa  fursa kwa wafanyabiashara kupata majibu ya haraka kuhusu changamoto zinazowakabili na kuongeza ushirikiano kati ya sekta binafsi na Serikali, jambo linaloendelea kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Singida.


Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MEI MOSI - MAJALIWA

    April 30, 2025
  • KIKWETE AFUNGA MICHEZO UWANJA WA CCM LITI

    April 30, 2025
  • "UMUHIMU WA MFUMO BORA WA USALAMA WA AFYA KAZINI"

    April 28, 2025
  • "UMUHIMU WA MFUMO BORA WA USALAMA WA AFYA KAZINI"

    April 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.