• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DIWANI WA MANISPAA YA SINGIDA AFARIKI DUNIA

Posted on: May 22nd, 2018

Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Unyamkwa Halmashauri ya Manispaa ya Singida Shabani Satu (CCM) amefariki dunia tarehe 18 mwezi huu katika Hospitali ya Ocean Road Dar-es-Salam alikuwa alikuwa anapata matibabu.

Taarifa ya CCM Wilaya ya Singida mjini ilieleza kuwa marehemu Satu ambaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani tangu mwaka 2016 alianza matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Singida na baadaye kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Muhimbili na Ocean road.

Taarifa hiyo imesema kuwa hicho ambachokimeleta huzuni na majonzi katika chama  hicho Halmashauri ya Manispaa na wananchi,kimeleta pengo kubwa kutokana na jinsi Satu alivyotegemewa na kutumainiwa ambaye mwili wake uliletwa Singida mjini kwa ajili ya mazishi.

Marehemu alizikwa  jana katika kitongoji cha Nambaro kijijini Kisasida baada ya mwili wake kufika  mjini Singida kusafirishwa kutoka nyumbani kwake mtaa wa Mnung’una Kata ya Minga huku Madiwani wa Manispaa hiyo wakibeba jeneza kuelekea makaburini wakishirikiana na mamia ya waombolezaji wakiongozwa na Shekh wa Wilaya hiyo Issa Ramadhani Simba.

Katka historia yake ili onyesha kuwa alizaliwa katika kitongoji cha Nambaro kijijini hapo tarehe 15 mwezi Novemba 1966 na kupata elimu ya msingi kuanzia 1977 hadi 1983 alipo hitimu, na baadaye kupata pamoja na shughuli zake za kujitegemea aliweza kukitumikia CCM na serikali yake kwa muda wa miaka 26.

Akisoma historia hiyo kwa niaba ya CCM na Halmashauri ya Manispaa hiyo, Diwani wa kata ya Utemini Baltazar Kimario alizitaja nafasi alizoshika marehemu kuwa ni ubalozi wa nyumba kumi, katibu wa tawi,mwenyekiti wa kitongoji cha Nambaro na Diwani wa Kata ya Unyambwa kwa vipindi vitatu hadi tarehe 18 Mei alipofikwa na umauti.

Akitoa salamu zake wakati wa mkusanyiko wa msiba huo mzitoambao ulihudhuriwa na waombolezaji wengi wakiwemo viongozi mbalimbali, Mstahiki meya Gwae Mbua, alionyesha masikitiko yake na kusema kuwamamlaka hiyo imeshiriki kikamilifu kumhudumia marehemu ambaye allikuwa hodari na mchangiaji mkuu katika maendeleo.

Mbua aliyeungwa mkono na viongozi wenzake wa  chama hicho na manispaa ya Singida alisema kuwa ushirikiano, upendo,viendelezwe katika kumuenzi marehemu na kuiga mfano wake kwa kufanya kazi pamoja na kutenda haki.

Pia katika salamu za Chama cha Mapinduzi Katibu mwenezi wa Wilaya ya Singida mjini Omari Shakarat alitoa pole kwa wanafamilia, ndugu,wanachama,Madiwani na watendaji wa mamlaka hiyo kwa kumpoteza Diwani hodari kipenzi cha watu aliyekuwa antumia muda wake ;kufanya kazi ya kutetea masilahi ya wananchi wake.

Aliwaomba wote kuwa na moyo wa subira katika kipindi hicho kigumu cha kupotelewa na marehemu kwa kudumisha upendo,umoja na ushirikiano.

Marehemu Shabani Satu ambaye kifo chake kimeleta majonzi makubwa na pigo kwa Halmashauri hiyo CCM na familia ameacha wajane wawili na kujaliwa kupata watoto tisa wakiwemo wakiume wanane, wakike mmoja na wajukuu watatu.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • INEC YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI

    May 14, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA VYA SIASA WALA KIAPO CHA UTII

    May 12, 2025
  • MANISPAA YA SINGIDA YATAKIWA KUPIMA MAENEO KABLA YA KUTEKELEZA MIRADI

    May 09, 2025
  • “PONGEZI KWAKO, RC HALIMA DENDEGO”

    May 09, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.