• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

ELIMU YA CHANJO ITOLEWE KWA JAMII ILI KUIKINGA NA MAAMBUKIZI YA MAGONJWA MBALIMBALI.

Posted on: April 24th, 2023

Wananchi wa Manispaa ya Singida wametakiwa kuzingatia chanjo kwa watoto wote walio na umri chini ya miaka mitano kutokana na umuhimu wake katika kudhibiti maambukizi ya magonjwa mbalimbali.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili wakati akizindua wiki ya chanjo kitaifa sambamba na kuweka jiwe la msingi katika zahanati ya Mtaa wa Isomia kata ya Mwankoko ambayo ni miongoni mwaka Kata zilizoko pepmbezoni mwa mji.

Mkuu wa Wilaya amehimiza wananchi wote wenye watoto wa umri chini ya miaka mitano kuhakikisha watoto hao, wanapata chanjo zote zinazostahili pamoja na mabinti wenye umri wa miaka 9 - 14 ambao wanapaswa kupata chanjo ya kuwakinga na saratani ya mlango wa kizazi.

“ niwahimize wananchi kupeleka ujumbe huu kwa jamii yote ili watoto waweze kupata chanjo zote stahiki… bila kuwasahau mabinti wenye umri wa miaka 9 - 14 ambao wanapaswa kupata chanjo ya kuwakinga na saratani ya mlango wa kizazi” amesisitiza Muragili na kuongeza kuwa, chanjo hizi ni bure na zinatolewa katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya.

Mhandisi Muragili amewataka wananchi kuondakana na dhana kuwa chanjo hizo zina madhara na kusisitiza kuwa chanjo zote zimefanyiwa utafiti wa kutosha kabla ya kuingizwa katika matumizi. Amesema chanjo zilianza miaka ya sabini ambazo zimeweza kuikinga jamii na maradhi mbalimbali yakiwemo ya ndui, surua, polio,kifua.

Mkuu wa wilaya katika kuhimiza umuhimu wa chanjo amemwagiza Mganga Mkuu wa Manispaa pamoja na timu yake kuweka ratiba ya kliniki kila wiki katika Mtaa wa Isomia kwa ajili ya watoto na wajawazito wakati kazi za ukamilishaji mradi wa zahanati hiyo ukiendelea na kwamba ifikapo Juni 30 atafika kwa ajili ya kukabidhiwa mradi.

Pamoja na uzinduzi huo, Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Muragili ameweza kuweka jiwe la msingi katika zahanati mpya ya Mtaa wa Isomia iliyojengwa kwa nguvu za wananchi  pamoja na serikali.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa Mradi huo wa zahanti, Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa, Dr. Hamis Yuna, amesema mradi huo ukikamilika utaweza kutoa huduma kwa wamama wajawazito na watoto katika jamii ya Isomia, lakini pia kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto pamoja na kupunguza umbali wa kufuata huduma ambao ni zaidi ya kilometa 6 hadi kufika zahanati ya  Mwankoko.

Dr. Yuna Amesema mradi huo hadi sasa umetumia zaidi ya  Tshs, Milioni 60 ambapo jumla ya wakazi 1,452  wa Mtaa wa Isomia watanufaika na mradi huu kati ya wananchi  7,624 wa kata  ya Mwankoko.

Pamoja na uwekaji wa jiwe la msingi Mgeni Rasmi Mhandisi Muragili aliweza pia kuendesha zoezi la upandaji miti ambapo vingozi mbalimbali wa chama na serikali pamoja na wananchi wameweza kupanda miti zaidi ya 60.

Manispaa ya Singida imeweza kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo usafi wa mazingira, kutembelea na kuweka jiwe la msingi katika moja ya miradi ya maendeleo, kupanda miti, uzinduzi wa chanjo, uchangiaji wa damu salama na mdahalo uliohusisha shule za sekondari ikiwa ni maadhimisho kuelekea kilele cha sherehe za miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.