• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

IPOSA KUONDOA UNYANYAPAA KWA VIJANA WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA MKOANI SINGIDA

Posted on: November 28th, 2023





Sekta ya  elimu mkoani Singida imetakiwa kubainisha na kuwasajili vijana wa kike na kiume ambao hawakubahatika kuingia katika mfumo rasmi wa elimu   Ili kuingizwa katika mpango wa elimu changamani (IPOSA).



Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga, ametoa wito huo Leo 28 Novemba, 2023 wakati akizindua mpango wa IPOSA mkoani Singida, uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo Cha Uhasibu, Singida.



Dkt. Mganga amesema, vijana wengi na hasa wa kike wamekuwa wakinyanyapaliwa kutokana na kukosa fursa ya kuingia katika mfumo rasmi wa elimu ama kushindwa kumaliza masomo baada ya kujiunga na mfumo huo, hivyo kupitia Mpango huo wa IPOSA, Unaotekelezwa baina ya serikali ya Tanzania na Korea Kusini, vijana hao waweza kupatiwa  elimu na ujuzi na hivyo kuweza kujiajiri na kujipatia kipato.



"Kutokujua kusoma na kuandika kunachukuliwa na wengine Kama njia ya udhalilishaji hasa Kwa mabinti na hivyo kusababisha unyanyapaa Kwa vijana hawa katika jamii", amesema Dkt Mganga.



Amesema, asilimia 21 ya wanafunzi waliomaliA darasa la Saba mkoani Singida 2023, hawajakidhi  kujiunga na elimu ya sekondari, hivyo kupitia IPOSA wataweza kunufaika na kujitegemea kupitia elimu na ujuzi watakaopata utakaowainia kiuchumi lakini pia kuchangia katika uchumi wa taifa .



Dkt. Mganga ametumia wasaa huo kutoa maelekezo Kwa Idara za Maendeleo ya Jamii katika halmashauri zote Saba za mkoa wa Singida, kuhakikisha zinashiriki vyema katika kuandaa vijana Kwa kuwapa mafunzo na ujuzi Ili kuwawezesha kujenga maisha bora.



Pamoja na Idara hiyo, ameitaka pia sekta ya elimu kuhakikisha watoto wote wanaosajiliwa kujiunga na elimu ya Msingi wanaendelea na masomo Bila kukatiza.



" Maafisa elimu Kata, hakikisheni mtoto anayesajiliwa katika kata yako hakatizi masomo yake Kwa sababu iwayo yoyote Ile", amesisitiza Dkt. Mganga



Aidha amewataka Kila mmoja katika Kata yake kuhakikisha anaendesha zoezi shirikishi la kuwabaini na kuwasajili vijana hawa Kwa kuwahusisha wakuu wa shule, walimu wakuu, maafisa Maendeleo ya Jamii na watendaji wa Kata.



Pamoja na maagizo hayo Katibu tawala huyo ametoa wito Kwa wadau mbalimbali kujitokeza Ili kushiriki katika kutokomeza suala Zima la watoto kutokujua kusoma na kuandika.



Mpango  wa elimu changamani (IPOSA) Unatarajiwa kutekelezwa  katika mikoa 6, mkoa wa Singida ukiwa ni miongoni mwa mikoa hiyo. Mikoa 10 ilishaanza utekelezaji wa mpango huo na kufanya jumla ya mikoa inayotekeleza kuwa 16.


Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.