• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KAMATI YA SIASA YA MKOA WA SINGIDA YATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO - UVIKO 19

Posted on: January 19th, 2022

Kamati ya siasa ya Mkoa wa Singida leo January 19, 2022 imeanza ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia fedha za UVIKO 19 pamoja na fedha za tozo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM inayotekelezwa mpaka mwaka 2025.

Akiongoza ziara hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa huo Alihaj Juma Kilimba alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua hali ya utekelezaji wa ilani ya chama kupitia fedha za UVIKO19 ambazo zimetumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na vituo vya afya sehemu mbalimbali mkoani hapa

Aidha, akiongea wakati wa ziara hiyo Alhaji Juma Kilimba ameshukuru viongozi mbalikmbali wa Chama na Serikali kwa usimamizi madhubuti wa ujenzi wa vyumba hivyo na kuwakumbusha kwamba walipewa fedha hizo kwa kuwa waliaminiwa na serikali ili kusimamia maendeleo kwa wananchi jambo ambalo amelitaka kuendelezwa.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo akatoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanakwenda shule kwa kuwa tayari kila shule ina vyumba vya madarasa na madawati ya kutosha huku akiwataka walimu kuongeza juhudi ya kufundisha kwa kuwa miundombinu ya elimu imeboreshwa kwa kiasi kikubwa.

Akipongeza serikali ya awamu ya sita, Alhaji Kilimba amesema kuwa serikali imekuwa ikitekeleza kazi zake kwa uwazi zaidi na kwa kasi kubwa huku akitolea mfano wa ujenzi wa miradi ya vyumba vya madarsa na vituo vya afya ambapo fedha za maendeleo zimekuwa zikija pamoja na maelekezo ya namna ya kuzitumia.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge amesema Mkoa wa Singida ulitengewa jumla ya Tshs. Bilioni 13.4 kwa ajili ya elimu msingi na sekondari kwa fedha zilizotokana na Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19.

Aidha Mkuu wa Mkoa akaendelea kusema kwamba kiasi hicho cha fedha kilitakiwa kujenga jumla ya vyumba vya madarasa 662 ambapo 330 ni vyumba kwa ajili ya shule za sekondari na 332 kwa ajili ya shule za msingi na vituo shikikizi.

Naye mjumbe wa kamati ya siasa ambeye pia ni Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili amesema katika wilaya yake kulikuwa na miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa 42 katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida na vyumba vya madarasa 67 katika Halmashauri ya wilaya ya Singida.

Aidha miradi mwingine iliyopokea fedha na kuendelea na utekelezaji ni pamoja na miradi ya afya na barabara ambapo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Changarawe eneo la kindai – unyianga- Mtamaa, ujenzi wa zahanati ya Unyianga na ujenzi wa kituo cha afya Mandewa ( Mwaja) alibainisha Mhandisi Muragili.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili akifafanua jambo mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Mkoa Alhaji Juma Kilimba na wajumbe wa kamati hiyo.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.