• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KAMATI YA SIASA YA WILAYA YARIDHISHWA NA UBUNIFU KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: July 10th, 2023

Kamati ya siasa ya wilaya ya Singida Mjini imeeleza kuridhishwa kwake na ubunifu uliotumika katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kupitia mradi wa BOOST na ile iliyotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Singida Mjini, Bi. Lucia Mwiru, ameeleza kuridhishwa na hali ya utekeleza wa miradi hiyo baada ya kukamilika kwa ziara iliyofanyika jana tarehe 10 Julai, 2023 katika Manispaa ya Singida ambapo miradi mbalimbali ikiwemo ya Afya, Elimu, Utawala, maji, barabara  na Vikundi vywa watu wenye ulemavu iliweza kutembelewa.

Mwiru ametoa pongezi kwa walimu wakuu na wakuu wa shule walioonesha ubunifu  katika miradi hiyo na kuwataka watekelezaji wengine kuiga mfano huo ambao ameuita ni wa KIZALENDO .

Pamoja na Pongezi hizo Mwenyekiti huyo wa  Chama Cha Mapinduzi Wilaya, amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe, kukaa na wataalamu ili kurekebisha kasoro zilizobainika katika miradi michache ikiwemo ya afya na ya elimu ili miradi iweze kukamilika na wananchi kunufaika nayo.

“Mkurugenzi kaa na wataalam wako muondoe kasoro chache tulizozibaini, tunataka miradi ikamilike na wananchi waweze kunufaika nayo”, amesisitiza Mwiru.

Hata hivyo mwenyekiti Mwiru, amemtaka Mkurugenzi kutosita kuchukuwa hatua kwa watumishi ambao wanahatarisha shughuli ya utekelezaji wa miradi kwa usimamizi duni na matumizi mabaya ya fedha za miradi.

Mwiru ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuona umuhimu wa kujenga mabwawa ya maji taka nakusema kuwa ujenzi huo utakapokamilika wananchi watanufaika nao kwa upande wa kilimo cha mbohgamboga na matunda na hivyo kukuza uchumi wao binafsi lakini pia kupendezesha mandhari ya Manispaa ya Singida .

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida,Yagi Kiaratu, akizungumzia ziara hiyo amesema ni utaratibu wa kawaida ambao unaboresha utendaji kazi wa watumishi katika halmashauri ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Aidha Mheshimiwa kiaratu ametumia fursa hiyo kama mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya, kuwapongeza wasimamizi wa miradi katika shule ya Msingi Kititimo, Minga na Mkuu wa Shule Mungumaji kwa kusimamia vizuri miradi na kuwa wabunifu hali iliyofanya thamani halisi ya fedha kuonekana katika utekelezaji wa Mradi hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Musa Sima, amepongeza walimu kwa usimamizi mzuri wa miradi ya BOOST na ile ya Serikali Kuu na kuwaasa watekelezaji wengine wa miradi inayoendelea na itakayokuja kuiga mfano mzuri wa walimu katika kusimamia miradi.

Aidha ameipongeza Serikali kwa kusikia kilio cha wananchi katika sekta za elimu, Afya, Maji na barabara kwa kupeleka fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi  hiyo katika Jimbo la Singida mjini na hivyo kupunguza changamoto zilizokuwa zinawakabili wananchi.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.