• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KONGOLE MANISPAA YA SINGIDA KWA KUFIKIA ASILIMIA 91 YA MAKUSANYO MAPATO YA NDANI

Posted on: May 9th, 2024



Wajumbe wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Singida wamepongeza juhudi kubwa iliyofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa pamoja na wataalam ya kusimamia vyanzo vya mapato na kukusanya mapato ya ndani kwa asilimia 91.

Pongezi hizo zimetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu pamoja na wajumbe wa baraza la madiwani leo Mei 09,2024  katika siku ya pili ya mkutano wa baraza hilo katika robo ya tatu, ulifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ufundi VETA, Manispaa ya SIngida.

 Meya ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza hilo amesema, mafanikio hayo ni matunda ya ushirikiano baina ya wataalamu na madiwani na kutoa rai kuendelea kushirikiana ili kuiwezesha halmashauri ya Manispaa kuvuka lengo ndani ya miezi miwili iliyobaki kabla ya mwaka kuisha.


Amesema pamoja na mafanikio hayo bado kuna baadhi ya vyanzo havifanyi vizuri na kuwataka wakuu wa Idara na vitengo ambao ni wasimamizi wa vyanzo vya mapato kuhakikisha kila mmoja anasimamia vyema chanzo chake ili kuweza kukusanya kadri ya malengo yaliyowekwa. 

“ wekeni utaratibu wa kujipima kwa siku, wiki na mwezi ili mbaini eneo lenye changamoto katika ukusanyaji mapato na kulitafutia ufumbuzi mapema”, amesema Kiaratu


Mstahiki Meya amezikumbusha idara zenye miradi inayoendelea kutekelezwa kuhakikisha zinaomba fedha za utekelezaji kulingana na mpango kazi wa utekelezaji mapema ili kuepuka changamoto ya mfumo kuzima ili kupisha ufungaji wa hesabu za mwaka jambo ambalo litasababisha kusimama kwa miradi.

Aidha amesisitiza juu ya ushirikishaji madiwani katika hatua zote za utekelezaji wa miradi kuanzia mapokezi ya fedha ,ujenzi na hata kukamilika kwa mradi na kukabidhi.

Naye wa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Bi Lucia Mwiru ameungana na wajumbe wa Baraza kupongeza bidii kubwa ya makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri iliyofanikisha kufikia asilimia 91 ya lengo la mwaka.

Aidha akizungumzia suala la miradi Mwenyekiti Mwiru,amewataka wataalam na hasa watendaji kuwashirikisha madiwani wa kata zao ambao ndiyo wenyeviti wa kamati za maendeleo za kata katika utekelezaji wa miradi kwa asilimia 100 ili kuleta tija katika miradi hiyo.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.