• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Mipangomiji
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu
      • Idara ya Maji na Usafi wa Mazingira
      • Idara ya Utumishi na Utawala
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAAFISA UGANI WATAKIWA KULETA MAPINDUZI YA KILIMO KATIKA MSIMU UJAO WA KILIMO 2022/2023

Posted on: June 13th, 2022

Maafisa Ugani mkoa wa Singida wametakiwa kuleta mapinduzi ya kilimo katika msimu ujao wa kilimo ili kukidhi mahitaji hususani ya chakula sambamba na ya viwanda.

Agizo hilo limetolewa leo (13/06/2022) na Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Binilith Mahenge wakati hafla ya kukabidhi pikipiki 166 kwa maafisa ugani na maafisa ushirika wa mkoa wa singida.

Alisema huko nyuma maafisa ugani walikabiliwa na changamoto sugu ya ukosefu wa usafiri hivyo kushindwa kuwafikia wakulima kwa wakati na kuwataka kutumika nyenzo hiyo kuwafikia wakulima, wafugaji na wana ushirika kwa muda muafaka na kutatua changamoto zinazohitaji utaalamu zinazowakabili.

Dr. Mahenge  amesema haitarajiwi wala haitavumiliwa kwa afisa yeyote wa ugani kutumia pikipiki aliyokabidhiwa tofauti na lengo kwa kuibadilisha matumizi na kuwa boda boda na atakayebainika,atachukuliwa hatua stahiki.

“Sasa tatizo la usafiri,limebaki kuwa historia.Pikipiki hizi zitumike kwa kufanyia kazi za Serikali za kuwafikia wakulima,wafugaji na wanaushirika.Hawa hakikisheni mnawapatia elimu ya kilimo bora,ufugaji wa kisasa na ushirika wenye tija.Tatueni chanagamoto zinazohitaji utaalamu wa ugani”,amesisitiza.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Singida amezitaka Halmashauri zote katika mkoa huo zihakikishe maafisa ugani wote wanapatiwa mafunzo ya udereva wa pikipiki ili kuepusha ajali zitokanazo na kukosa elimu ya udereva na kwamba mafunzo hayo yafanyike kabla ya mwezi huu kuisha. Amewataka waafisa hao wahakikishe wanazitumia pikipiki hizo kwa uagalifu mkubwa, ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.

“Wakurugenzi wa halmashauri ninasisitiza kufuatilia matumizi sahihi ya pikipiki na kuchukua hatua stahiki mapema kwa maafisa watakaotumia pikipiki kinyume na maelekezo haya”, amesema.

Pia amewataka maafisa ugani kuandaa mpango kazi wa kila siku, anapotumia pikipiki ifahamike wazi amekwenda wapi,amehudumia wateja wangapi ambao ni wakulima, wafugaji, AMCOS na SACCOS.

“Pikipiki zilete madadiliko chanya katika kilimo,mifugo na ushirika” na akatoa rai kwa  Maafisa ugani kuwafikia na kuwapatia mafunzo wateja wengi zaidi na kwamba tija ya mafunzo hayo ionekane katika kuongezeka kwa matumizi ya kanuni bora na uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo hasa zao la alizeti ambalo ni zao la kimkakati kimkoa lipewe kipaumbele.

Halmashauri ya Manispaa ya Singida imepokea jumla ya pikipiki 14 zitakazo hudumia kata zote 18 za Manispaa ya Singida.

Matangazo

  • TANGAZO LA UPANGAJI UPIMAJI NA URASIMISHAJI WA MAENEO KWA NJIA SHIRIKISHI June 16, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI March 07, 2022
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA MANISPAA YA SINGIDA KWA SHULE 2021 November 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA MANISPAA YA SINGIDA KWA KATA 2021 November 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • WANANCHI MANISPAA YA SINGIDA WAPONGEZA JITIHADA ZA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KATIKA KUSOGEZA HUDUMA KARIBU NA WANANCHI

    June 23, 2022
  • RC SINGIDA: SIMAMIENI VIZURI VYANZO VYA MAPATO ILI KUPUNGUZA HOJA ZA UKAGUZI

    June 15, 2022
  • WATUMISHI MANISPAA YA SINGIDA WAASWA KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA

    June 14, 2022
  • WATUMISHI MANISPAA YA SINGIDA WAASWA KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOWEA

    June 14, 2022
  • Tazama Zote

Video

Waziri Jafo atoa maagizo mazito kwa ma-RAS, ma-DED, Wakuu wa idara na maasifa mawasiliano serikalini
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.