• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SINGIDA YATOA MAFUNZO KWA WADAU MBALIMBALI JUU YA ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI

Posted on: March 3rd, 2022

Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Mulagiri amesema zoezi la uandaaji anwani za makazi na postikodi ni zoezi linalohitaji ushikishwaji wa hali ya juu katika ngazi zote hususan ngazi inayohusu mwananchi moja kwa moja ilifufanikisha kazi hiyo na kuwataka washiriki kuwa makini ili kuepuka dosari zinazoweza kupelekea kuharibu utekelezaji wa zoezi hilo

Amesema kwa uhabarisho waliopatiwa wadau leo ni heshima ya kipekee kwani wao wamekuwa washiriki wa moja kwa moja katika nafasi zao katika kutekeleza zoezi la uwekaji wa anwani za makazi na kwamba uwepo wa Viongozi mbalimbali, wenyeviti wa mitaa watendaji ni wazi kuwa zoezi la uwekaji anwani za makazi linakwenda kufanikiwa .

Alisema zoezi hili ili liweze kufanikshiwa vizuri na kuweza kuonekana katika kiwango kinachotakiwa kunagharama kubwa zitakazotumika na ni zoezi ambalo haliepukiki. Ameendelea kufafanua kuwa zipo gharama zitakazobebwa na Serikali kuu, Manispaa na wananchi wenyewe nakuwataka wadau wasiogope kwani ni jukumu letu sote na linamanufaa makubwa kwa Jamii

“ msiogope ukubwa wa gharama hizi kwani gharama hizi zikishushwa katika ngazi ya mwananchi gharama hizo sio kubwa” alisisitiza Mkuu wa wilaya na kuwataka wananchi kuchangia kwa kununua kibao kidogo cha namba kwa ajili ya kupachika katika nyumba zao.

Aidha Mhandisi Mulagiri aliendelea kuwaomba wenyeviti wa mitaa Pamoja na wananchi katika mitaa yao kubebba gharama za kusimika nguzo na vibao katika mitaa yao badala ya kuiachia Serikali pekee nakuongeza kuwa serekali itabeba gharama za vibao vinavyoonesha barabara.

“kama Serikali hatuwezi peke yetu kuweka vibao katika mitaa yote, ndio maana nawaomba tusaidiane hizi gharama, Serikali itabeba sehemu yake, Manispaa vilevile Mtaa na mwananchi mmoja mmoja”alisihi Mkuu wa wilaya.

Mkuu wa wilaya aliwasisitiza wenyeviti  wa mitaa kuhakikisha elimu / uhabarisho walioupata wanaufikisha vyema kwa wananchi ili kufanya zoezi hili kuwa rahisi na kuwataka kuhakikisha wanafanya kazi ya kugawa madodoso kwa umakini na uaminifu mkubwa bila kumwacha mkaazi katika mtaa wake.

“inawapasa kufanya kazi hii kwa uaminifu na umakini mkubwa, msifanye kosa la kumwacha mtu bila kumpatia dodoso haijalishi mida anayorudi nyumbani hakikisheni anapatiwa dodoso na anajaza taarifa zake” alisisitiza

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mhe. Yagi Kiaratu ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya katika ufunguzi wa mafunzo/ uhabarisho alisema Manispaa imetambua umuhimu wa wadau mbalimbali kushirikishwa katika zoezi la uwekaji anuani za makazi na postikadi ili kuifanya kazi hii kuwa shirikishi na hivyo kuleta wepesi katika utekelezaji.

Alisema Mpango huu una manufaa mengi  ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi  katika utawala bora kwa kutambua makazi ya raia wote nchini, kuimarisha usalama, kuboresha utoaji huduma za Jamii na kuongeza pato la taifa kwa kuboresha ukusanyaji wa kodi mbalimbali

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida Mjini Bi. Lucia Mwiru alimpongeza mstahiki meya pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi kupitia kamati ya kuratibu zoezi la uwekaji anwani za makazi kwa kuandaa mafunzo/ uhabarisho kwa wadau na kusema kuwa kwa sura hii Halmashauri ya Manispaa ya Singida itafanikiwa kwa asilimia kubwa katika utekelezaji wa zoezi hili.

“ hii ni halmashauri ya  kwanza kufanya uhabarisho kwa Viongozi mbalimbali,  wenyeviti wa mitaa, watendaji  wa kata na Mitaa Pamoja na wadau mbalimbali  hii inamaana kwa kuwa tumeanza mapema basi na zoezi letu litakwenda vizuri sana” alipongeza  Bi. Mwiru

Jumla ya wadau 275 wakiwemo waheshimiwa madiwani, Viongozi wa dini, wazee maarufu, wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama wilaya, wenyeviti wa mitaa na  Vijiji, Wakuu wa idara na Vitengo, wawakilishi wa taasisi mbalimbali, watendaji wa kata, mitaa na Vijiji, walimu Wakuu, Wakuu wa shule na Maafisa elimu Kata walishiriki mafunzo hayo.

Matangazo

  • NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA SINGIDA June 03, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • VIKUNDI 55 VYAPATIWA MAFUNZO KABLA YA KUPOKEA MIKOPO YA 10%

    June 29, 2025
  • SINGIDA MANISPAA YAANZA KUTOA ELIMU YA UCHAGUZI MKUU KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • USAFI WA NGUVU KUELEKEA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA WAFIKIA ASILIMIA 80

    June 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.