• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA SINGIDA YAANDIKISHA ZAIDI YA ASILIMIA 78 ELIMU YA MSINGI 2025

Posted on: January 13th, 2025

Jumla ya wanafunzi 4,237 wameandikishwa kuanza elimu ya awali, kati ya 7,034 waliokusudiwa, katika shule mbalimbali za Manispaa ya Singida, na wengine 5,251 wakiandikishwa darasa la kwanza, kwa muhula wa masomo ulioanza leo Jumatatu, tarehe 13Januari, 2025, kati ya watoto 6,670 waliotarajiwa mwaka huu.

Kaimu Afisa Elimu awali  na msingi Manispaa ya Singida, Mwalimu Beno Magesa amesema kuwa, hadi kufikia siku ya kwanza ( leo Jumatatu), uandikishaji wanafunzi wa awali ni sawa na asilimia 52.24, wakiwemo wasichana 2,325, kati ya 3,592 ya waliokusudiwa na wavulana 2112 waliandikishwa sawa na asilimia 62.36 kati ya 3442 waliotarajiwa.

“Wanafunzi wa awali,mpaka shule zinafunguliwa kuanza muhula wa masomo, Manispaa imeandikisha wanafunzi 4,237 kati ya maoteo ya 7,034, wakiwemo wasichana 2,325 na wavulana 2,112…naamini idadi hii itaongezeka, kwa wazazi kuandikisha watoto wao, wakati masomo yakiwa yanaendelea darasani,”alisema Magesa.

Kuhusu uandikishaji wanafunzi wa darasa la kwanza, Mwalimu Magesa alifafanua kuwa, hadi kufikia siku ya kwanza ya muhula wa masomo, tayari wanafunzi 5,251 sawa na asilimia 78.73 wameandikishwa, kati ya 6,670, ya waliokusudiwa.

Alisema kuwa, kwenye idadi hiyo wapo wasichana 2,545 ambao ni sawa na asilimia 75.45, na wavulana 2,706, sawa na asilimia 82.7 ya waliokusudiwa.

Kaimu afisa elimu huyo, alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi na walezi wenye watoto ambao bado hawajaandikishwa, wahakikishe wanawapeleka katika shule zilizopo jirani na maeneo yao, ili wanafunzi waweze kutumia haki yao ya msingi ya kupata elimu inayotolewa bure na serikali yao.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Dk. Samia Suluhu Hassan, Bi. Jasmini Nkinga, alisema hadi kufikia leo Januari 13, 2025 wakati shule zinafunguliwa, amekwishapokea wanafunzi 135 wa awali na wengine 132 wa darasa la kwanza, huku lengo likiwa kila darasa kuwa na wanafunzi 200.

Hata hivyo Mwalimu Nkinga amefafanua kuwa, pamoja na kujiwekea lengo la kila darasa kuwa na waafunzi 200, lakini wakijitokeza zaidi, uongozi hautakuwa na pingamizi lolote, zaidi ya kuwapokea tayari kwa ajili ya kuwapatia haki yao ya msingi, ambayo ni elimu.

Kadhalika Mwalimu Nkinga amewaomba wazazi na walezi kutumia vema fursa hiyo muhimu, na wahakikishe wanajitahidi kuwapatia mahitaji muhimu ya sare, ili kuwatoa hofu na uonyonge watoto wao, hasa pale wanapochanganyika na wenzao wenye sare zinazopendeza na kuvutia.

Matangazo

  • NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA SINGIDA June 03, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • VIKUNDI 55 VYAPATIWA MAFUNZO KABLA YA KUPOKEA MIKOPO YA 10%

    June 29, 2025
  • SINGIDA MANISPAA YAANZA KUTOA ELIMU YA UCHAGUZI MKUU KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • USAFI WA NGUVU KUELEKEA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA WAFIKIA ASILIMIA 80

    June 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.