• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SINGIDA IMEPONGEZWA KWA KUVUKA LENGO LA UKUSANYAJI MAPATO KIPINDI CHA ROBO YA PILI 2023

Posted on: March 7th, 2023

Wajumbe wa Baraza la Madwani la Halmashauri ya Manispaa ya Singida, wamepongeza juhudi zinazofanywa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa, katika suala zima la ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kipindi cha Januari- March 2023.

Wajumbe wa Baraza hilo wametoa pongezi hizo leo tarehe 07/03/2023 katika mkutano wa robo ya pili wa Baraza hilo, wakati wakijadili taarifa mbalimbali za kamati.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Maulid Kiaratu , amesema Halmashauri yake, kwa mwezi Januari, 2023 imefanikiwa kukusanya mapato kwa aslimia 104 na kutoa rai kwa wataalam kuendelea kusimamia kwa bidii ukusanyaji wa mapato kwani kipindi cha Januari na Februari ni “ low season”, kwa wafanyabiashara.

Meya Kiaratu,amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa kufanyia kazi mapendekezo/ ushauri uliotolewa ikiwa ni pamoja na kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato.

Aidha Mstahiki ametanabaisha kuwa kupitia asilimia 10 za mapato ya ndani, zaidi ya Shilingi milioni 400,000,000/- zimetolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Amesisitiza idara ya maendeleo ya jamii kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya fursa za uwezeshwaji kiuchumi zilizopo ili wananchi waweze kutumia nafasi hizo.

Akijibu swali la papo  kwa papo lililohusu mkakati wa Manispaa katika kukusanya mapato ya vitunguu kwa kuwa msimu wa 2023 umekaribia, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe , amesema Manispaa imejipanga vyema kwani tayari imefanya mazungumzo na uongozi wa soko na wameweka mikakati madhubuti ili kuhakikisha mapato hayachepushwi.

Akichangia mjadala Mhe. Geofrey Mdama, Diwani wa Kata ya Unyianga ametoa pongezi kwa manispaa kutokana na ukusanyaji mzuri wa mapato na kusema kuwa ni matokeo ya usimamizi thabiti wa kamati ya fedha na Utawala pamoja na timu nzima ya menegimenti ya Manispaa.

Naye Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Martha Gwau, amepongeza ushirikiano baina ya madiwani na timu ya menejimenti na kusema ushirikiano huo ndio nguzo ya kuinua Manispaa ya Singida kufikia malengo yake.

Aidha Gwau amepongeza pia jitihada za Manispaa za utoaji mikopo ya asilimia 10 ya  fedha za mapato ya ndani na kuongeza kuwa hiyo ni kutokana na uongozi wa Manispaa kuthamini na kutambua umuhimu wa kuwezesha wananchi kiuchumi.

Kwa upande wake Naibu Meya Hassan Mkata, amehimiza ushirikiano katika usimamizi wa mapato na kuongeza kuwa, manufaa ya mapato ya ndani yameonekana ambapo ametaja baadhi ikiwa ni pamoja na ununuzi wa gari mbili za kubeba taka, ujenzi wa kituo cha Afya Mtipa pia matengenezo ya mtambo wa kuzolea taka ambao ulikuwa umesimama kwa muda mrefu.

Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Musa Sima, pia ameipongeza Manispaa kwa jitihada za ukusanyaji mapato na kutoa rai kwa Mkurugenzi kufanya ufuatiliaji wa miradi ya kimkakati kupitia Benki ya Dunia (TACTIC) OR-TAMISEMI, ili Manispaa iweze kufaidika  kwani ni moja kati ya halmashauri 45 zitakazonufaika na mradi huo.

Matangazo

  • MAPITIO YA BAJETI 2022/2023 February 21, 2023
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA MANISPAA YA SINGIDA KWA SHULE 2021 November 15, 2021
  • KARIBU UWEKEZE KATIKA MANISPAA YA SINGIDA November 15, 2022
  • TATHMINI YA MATOKEO YA MITIHANI YA DARASA LA SABA 2022 KI- SHULE December 23, 2022
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • KAYA 5,396 MANISPAA YA SINGIDA ZIMENUFAIKA NA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF) DIRISHA LA SEPTEMBA - OKTOBA, 2023

    March 22, 2023
  • BOT YATOA ELIMU YA FEDHA BANDIA KWA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA KIMATAIFA LA VITUNGUU, MISUNA MANISPAA YA SINGIDA

    March 20, 2023
  • TUME YA UTUMISHI YA WALIMU SINGIDA YAWATAKA WALIMU KUZINGATIA SHERIA,KANUNI NA MIONGOZO INAYOTOLEWA NA SERIKALI

    March 20, 2023
  • MIAKA MIWILI YA DHAHABU YA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN YALETA MAPINDUZI YA MAENDELEO SINGIDA

    March 18, 2023
  • Tazama Zote

Video

Waziri Jafo atoa maagizo mazito kwa ma-RAS, ma-DED, Wakuu wa idara na maasifa mawasiliano serikalini
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.