• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SINGIDA KATIKA WIKI YA MAADHIMISHO KUELEKEA KILELE CHA MIAKA 59 YA MUUNGANO

Posted on: April 20th, 2023

Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wananchi wa Manispaa ya Singida wamefanya zoezi la usafi katika Soko la Kimataifa la Vitunguu, ambalo uwepo wake umetajwa kama moja ya faida  ya Muungano.

Akiongea na wananchi baada ya ya kukamilisha zoezi la usafi lililoanza leo tarehe 20 April, 2023 saa 12:30 asubuhi, Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili, amewataka wananchi hao kuuenzi Muungano kwa kuulinda na kuutetea kwa kudumisha amani iliyopo ambayo ni matokekeo ya muungano huo.

Muragili amesema wananchi wa Singida wana kila sababu ya kuulinda Muungano huo kutokana na amani na utulivu uliopo jambo ambalo nchi nyingine hazina amani hiyo .

Akizungumzia uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano,  Mkuu wa wilaya ya Singida amesema ,uzinduzi huo umefanyika kwa kufanya usafi ikiwa ni ujumbe mahususi kwa wananchi wote ya kwamba Manispaa ya Singida imejipanga kuwa safi na pia kuwa miongoni mwa miji bora kwa usafi nchini.

“ tumekwisha amamua na tumejipanga kuwa usafi sasa utafanyika katika maeneo yote ya makazi yetu na maeneo ya biashara….usafi wa mara moja kwa mwezi tunaachana nao badala yake utafanyika ni kila siku”, amesema Muragili.

Amewataka wananchi kulipa ada ya taka ili kuiwezesha Halmashauri ya Manispaa kuzoa taka na kupeleka dampo nje ya mji na kuongeza kuwa gharama za uzoaji taka ni kubwa kotakana na uzalishaji mkubwa wa taka uliopo, hivyo serikali peke yake haitamudu pasipo kushirikiana na jamii.

Aidha amesema kila mwananchi ahakikishe anafuata ratiba na kutoa taka nje ya nyumba ili ziweze kubebwa na kupelekwa dampo badala ya kutupa kwenye vizimba hali inayoongeza gharama ya uzoaji.

“….kila kaya inazalisha taka hivyo ni wajibu wa kila kaya kulipa ada ya taka ambayo ni shilingi 2,000 kwa mwezi na atakayekaidi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kwani suala hili sio hiari”, amesisitiza Mkuu wa Wilaya.

Manispaa ya Singida imepanga kutekeleza shughuli mbalimbali katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar . Shughuli hizo ni pamoja na kutembelea miradi ya maendeleo na kuweka mawe ya msingi, upandaji miti, kuendesha mtahalo juu ya Historia na mafanikio ya muungano pamoja uchangiaji damu salama ambayo ni moja ya huduma za kijamii.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.