• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TUJENGE UTAMADUNI WA KUWAENZI WANANCHI WALIOTOA ARDHI KWA AJILI YA SHUGHULI ZA MAENDELEO

Posted on: July 31st, 2023

Katika kuwathamini wananchi wake, Manispaa ya Singida, imekusudia kuandaa hafla ya kuwatuza wote walijitolea ardhi kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.

Hayo yameelezwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Maulid Kiaratu, kwenye hafla ya kukabidhi shule  mpya ya msingi Imbele, ujenzi uliotekelezwa kupitia mradi wa BOOST.

Mstahiki Meya alitoa ahadi hiyo, baada ya Mbunge wa Singida mjini, Mussa Sima, kumtambulisha mama Kisanga Imbele na familia yake ambao wametoa eneo, lilitumika kujenga shule hiyo mpya.

“Kwa kuthamini wananchi waliojitolea ardhi yao kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ikiwemo shule, zahanati na vituo vya afya, Manispaa itaandaa hafla ya kuwatuza na kuwaenzi wananchi hao, pamoja na kuwapatia vyeti vya heshima, ambavyo vitakuwa kumbukumbu nzuri kwa Manispaa ya Singida” amesema Meya.

Mhe. Kiaratu ameendelea kufafanua kuwa kwa kuwaenzi na kuwatuza wananchi hawa, kutakuwa ni mfano mzuri kwa wengine hasa wale wanaojitolea maeneo yao kwa kazi za maendeleo na baadaye kuanza kudai fidia.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo, Mussa Sima, ameunga mkono tamko la Mstahiki Meya la kuwaenzi wananchi wazalendo waliotoa maeneo yao kwa ajili ya shughuli za maendeleo .

Katika kumpongeza mama Imbele,Mbunge Sima aliwaongoza viongozi na wananchi walioshiriki hafla hiyo ya makabidhiano, kumtuza fedha taslimu hali iliyopokelewa kwa furaha, kutokana na mwitikio mkubwa wa viongozi na wananchi waliohudhuria hafla ya kupokea mradi huo wakiwemo wanafamilia ya Imbele.

“Wananchi kama hawa, wana kila sababu ya kuenziwa, kutokana na uzalendo na upendo walioonesha kwa nchi yao, jambo linalopaswa kuigwa,” amesema Mbunge.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.