• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SINGIDA YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA GIRL GUIDE TANZANIA

Posted on: June 4th, 2022

Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa kushirikianana taasisi isyo ya kiserikali ya Girl Guide Tanzania na wananchi wa Kata ya Kindai, wameadhimisha siku ya Mazingira Duniani leo tarehe 4 June, 2022 kwa kufanya usafi katika eneo linalozunguka uwanja wa mpira wa Namfua ikiwa ni njia mojawapo ya kuhamasisha Jamii kujenga tabia ya usafi katika maeneo wanayoishi ama kufanyia shughuli zao mbalimbali.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa Bi. Theresia John ambaye pia ni Afisa Mazingira amesema ujumbe wa Mwaka huu  ni “TANZANIA NI MOJA TU, TUTUNZE MAZINGIRA” hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anatunza mazingira yanayomzunguka iwe ni nyumbani ama katika biashara.

Amesema wapo watu ambao hawafanyi usafi mpaka kusimamiwa na kuonya kuwa wahakikishe wanatii sheria bila shuruti kwani suala la uchafuzi wa Mazingira halina msamaha.

“Uchafu unaozalishwa na mtu mmoja huathiri watu zaidi ya mia moja kwani huweza kusababisha mlipuko wa magonjwa”, amesema Bi. Theresia

Naye Mwenyekiti wa Girl Guide Mkoa wa Singida Bi. Anitha Msangi alisema taasisi hiyo inayojishugulisha na elimu ya maadili mema kwa mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla,  imeona vyema kushirikiana na jamii kufanya usafi ikiwa ni njia moja wapo ya kuelimisha jamii kuhusiana na masuala ya usafi kwa kupenda mazingira yaliyo safi kwa usalama kwa afya zao.

“Girl Guide tumeona vyema kushiriki maadhimisho haya kwa pamoja ili tuweke singida yetu safi” alisema Bi. Msangi na kuongeza kuwa wanachama walioshiriki wa girl Guide ni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ikungi, na Manispaa ya Singida.

 Mwenyekiti wa Mtaa wa Dodoma Road Ndg. Maulid Ramadhani  amesema zoezi hilo la usafi katika eneo la Namfua linapswa kufanyika kwa nguvu zote na kwa kuweka tozo za juu ili kila mwenye shughuli eneo hilo awajibike kwa usafi na kwamba eneo hilo ni uso wa mji wa singida.

“Magari mengi hupumzika hapo kabla ya kuendelea na safari hasa malori, hivyo bila kuweka faini kubwa uchafunzi wa mazingira utakuwa mkubwa sana” alisema.

Manispaa ya Singida hufanya shughuli ya usafi kila mwisho wa wiki (Jumamosi) ambapo wananchi katika makazi yao na maeneo ya biashara huwajibika kufanya usafi wa kina ambapo maeneo yote ya biashara hufungwa mpaka muda wa saa tatu asubuhi ndipo hufunguliwa baada ya usafi kukamilika.

Zoezi hili la usafi ni mwendelezo wa kampeni ya usafi wa Mazingira iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Binirith Mahenge 30 Oktoba, 2021 ya kuuweka Mkoa wa Singida katika hali ya usafi na mandhari ya kupendeza.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • KONGOLE MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUPEWA TUZO MAALUM YA HESHIMA NA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    May 31, 2025
  • Meya atoa onyo kwa wasiotunza mazingira Manispaa ya Singida

    May 31, 2025
  • MKURUGENZI WA MANISPAA AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI MKOA WA SINGIDA

    May 30, 2025
  • WANANCHI 35 WAFANYIWA UPASUAJI WA MTOTO WA JICHO SINGIDA

    May 29, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.