• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SINGIDA YAANZA UJENZI WA OFISI ZA WAFANYABIASHARA WADOGO - MACHINGA

Posted on: May 2nd, 2023

Halmashauri ya Manispaa ya Singida leo  tarehe 2 Mei, 2023 imezindua ujenzi wa jengo la ofisi za wafanyabiashara wadogo (Machinga) kufuatia fedha zilizotolewa na serikali kuu shilingi milioni 10 kwa ajili ya ujenzi huo ili kuwezesha wafanyabiashara hao kufikika wakati wote.

Akizindua ujenzi wa ofisi hizo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida , Yagi Kiaratu, amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia wafanyabiashara hao kufikika kirahisi kupitia uongozi wao, ambao sasa watakuwa na sehemu ya kuendeshea shughuli zao za kiutawala na kutatua kero za wadau wao.

“ uwepo wa ofisi hii utanufaisha pande zote , kwetu kama serikali tukitaka kujadiliana nanyi masuala ya mbalimbali ya maendeleo tunajua mahali pa kuwapata, lakini pia kwenu katika kuwahudumia wanachama wenu wanajua mahali pa kuwapata”, amesema Meya wa Manispaa

Uzinduzi huo ambao ulishirikisha Uongozi wa Manispaa, wakuu wa idara na vitengo, Uongozi wa Kata na Mtaa, viongozi wa wafanyabiasahara wadogo maarufu kama machinga na Uongozi wa waendesha bodaboda na bajaji, umefanyika kwa  shughuli ya uchimbaji Msingi, ambao utasaidia kupunguza gharama ya ujenzi kutokana na msingi huo kuchimbwa na jamii badala ya fundi.

Akisoma taarifa ya mchakato wa ujenzi wa ofisi hizo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Jeshi Lupembe amesema, Manispaa ya Singida imepokea fedha kiasi cha Tshs. Milioni 10 kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida, kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Machinga fedha ambazo zimetolewa na serikali kuu.

Jeshi amesema Halmashauri ya Manispaa imeanza ujenzi wa ofisi hizo mtaa wa Uwanja wa Ndege Kata ya Mandewa katika eneo lililotengwa kwa shughuli za soko,  maarufu kama Soko la Mahinya, ili kutoa nafasi kwa machinga kutumia eneo hilo kwa shughuli za biashara sambamba na ofisi ili kurahisisha utoaji huduma kwa walengwa bila usumbufu.

Amesema Manispaa imepanga kurasimisha eneo hilo kwa shughuli za gulio la kila wiki ili wafanyabiashara wadogo waweze kuendesha biashara zao kwa uhuru na nafasi. Na kuongeza kuwa uwepo wa gulio la kila Ijumaa litaongeza thamani ya eneo hilo lakini pia kutanua mji.

Kaimu Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa ujenzi wa ofisi hizo unatarajia kugharimu kiasi cha Tshs. Milioni 46 hadi kukamilika kwake na hivyo kutoa rai kwa sekta binafsi kushirikiana na serikali kukamilisha mradi huo wenye manufaa kwa wananchi wote.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Viwanda,Biashara na uwekezaji, Eric Sinkwembe, amesema uwepo wa ofisi ya wafanyabiashara wadogo na watoa huduma wadogo wa usafiri  (bajaji na bodaboda) ni faraja kubwa na kwamba changamoto zilizokuwa zikiwakabili wadau ya kukosa eneo la kukutania  sasa zimetatuliwa.

Amesema awali, wadau hao walikuwa wakilazimika kukutana sehemu isiyorafiki  ili kujadiliana masuala yao lakini kwa sasa changamoto hiyo imepata ufumbuzi kwani watakutana eneo rasmi kwa kusikilizwa na kutatua changamoto zinazowakabili.

“ kwa sasa hivi ili mdau aweze kusaidiwa ni lazima amtafute kiongozi kwa simu au amfuate eneo lake la biashara hivyo kusababisha usumbufu”, amesema Sinkwembe

Wakiongea kwa niaba ya wamachinga Mwenyekiti wa Machinga Ismail Otta na Makamu mwenyekiti  Bi. Asha Shaban, wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza ahadi yake ya kutoa eneo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Machinga katika kila mkoa, ahadi aliyoitoa katika kikao chake na viongozi wa machinga jijini Dodoma.

Aidha viongozi hao wameishukuru serikali pia kwa kuwatambau wamachinga kama kundi maalum na kwamba sasa wanaweza kukaa meza moja kujadili chngamoto mbalimbali bila mvutano wowote.

Pamoja na Shukrani hizo wameupongeza Uongozi wa Manispaa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Jeshi Lupembe, kwa ushirikiano wanaoutoa kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa manufaa ya Mchinga  lakini pia manufaa ya Manispaa ya Singida

Kata ya Mandewa ni moja ya kata zenye maeneo mengi yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji yakiwemo maeneo kwa ajili ya masoko,na  taasisi za umma .

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.