• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SINGIDA YAONGOZA KIMKOA KATIKA UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST

Posted on: July 30th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, ameitakangaza Manispaa ya Singida kuwa kinara katika utekelezaji wa mradi wa Boost na kusema miradi iliyotekelezwa katika Manispaa hiyo imezingatia viwango vya ubora katika majengo yake.

Serukamba amesema hayo leo tarehe 30 Julai, 2023 wakati wa hafla ya makabidhiano ya miundombinu ya  elimu iliyojengwa kupitia mradi wa BOOST  mwaka 2022/2023, iliyofanyika katika Shule Mpya ya Msingi ya Imbele , Manispaa ya Singida.

Mkuu wa Mkoa amesema pamoja na kumaliza ujenzi kwa wakati, Manispaa ya Singida imeongoza kwa kujenga majengo yenye ubora na yaliyozingatia vigezo.

Halmashauri iliyofuatia ni Mkalama iliyoshika nafasi ya pili, Halmashauri ya wilaya ya Singida nafasi ya tatu, ikifuatiwa na Halmashauri ya Manyoni nafasi ya nne na Itigi nafasi ya tano. Nafasi mbili za mwisho zimeshikwa na Halmashauri ya Iramba na Ikungi ambazo zilishindwa kukamilisha kwa wakati kutokana na changamoto mbalimbali.

Serukamba amesema, Mkoa wa Singida ulipatiwa zaidi ya shilingi Bilioni 9.2 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Boost ambapo jumla ya madarasa 305, matundu ya vyoo 420, matundu ya vyoo vya kisasa 72 kwa ajili ya shule za awali, nyumba za walimu 02 na majengo ya utawala 12 yamejengwa.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amebainisha pia kuwa miongoni mwa miundombinu hiyo zipo shule mpya 12 za msingi zilizojengwa  katika halmashauri zote saba za Mkoa wa Singida, ambapo alisema hayo ni mafanikio makubwa ya kujivunia.

Serukamba amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kugusa maisha ya wananchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, afya, maji, umeme, barabara , kilimo na kuwataka wananchi wa mkoa wa Singida kumuombea Rais afya njema aweze kufanya mengi zaidi kwa ajili ya watanzania.

“…ukizunguka nchi hii, kila kijiji utakachoenda kuna mradi unaendelea,…..kwa kipindi cha miaka miwili alichokaa madarakani Rais Samia amejenga shule zaidi ya 1000…..” amesema Serukamba.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida,  Mhandisi Paskasi Muragili akiwasilisha taarifa ya mradi wa Boost katika wilaya ya Singida kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa kuitoa Singida kimasomaso na hususan wilaya ya Singida yenye Halmashauri mbili kupitia mradi wa boost.

Amesema  kupitia mradi huu wa Boost, jumla ya wanafunzi 2,745 wa shule ya msingi  katika Manispaa ya Singida, watanufaika kutokana na uwepo wa vyumba vya madarasa 61 vipya, vyoo matundu 49, vyumba vya madarasa ya awali  6, matundu ya vyoo vya kisasa 18 vya madarasa ya awali na majengo 02 ya utawala.

Amesema uwepo wa miundombinu hiyo ya kujifunzia sio tu itapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa wanafunzi madarasani lakini pia kuwawezesha wanafunzi hao kufuatilia masomo kwa utulivu kutokana na uwepo wa samani / madawati kulingana na idadi ya wanafunzi katika vyumba vya madarasa hayo mapya.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Fatma Mganga, ametoa pongezi kwa Rais  wa awamu ya sita , Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa kujali wananchi wake na kusema wanawake tuna kila sababu ya kujivunia uwepo wake katika nafasi hiyo.

Dkt. Mganga pia amewapongeza walimu na watendaji ambao wamevaa viatu vya wahandisi kwa kusimamia vyema mradi wa Boost na kuwaasa kuwa kazi iliyobaki ni kuleta matokeo mazuri ya ufaulu kwa wanafunzi.

Katibu Tawala amezitaka halmashauri kuwajengea uwezo mafundi  katika jamii ( Local Fundi’s) ili kuboresha uwezo wao katika shughuli za ukamilishaji wa ujenzi wa majengo ili kazi hizo ziweze kuwa na ubora.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini,Mussa Sima, ametoa shukrani za kipekee kwa  Serikali ya awamu ya Sita na kusema wananchi wa Singida Mjini wana deni kubwa kwa Mheshimiwa Rais kutokana na maendeleo aliyoyaleta katika mkoa wa Singida na hasa katika Manispaa ya Singida.

Amesema pamoja na Mradi wa Boost lakini pia miradi ya ukamilishaji wa miundombinu kwa ajili ya kidato cha tano katika sekondari ya mandewa maalumu kwa wasichana, ujenzi wa shule mpya ya sekondari  kata ya Utemini,  na ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Uhamaka  inaendelea.

Mhe. Sima ametumia fursa hiyo pia kuishukuru familia ya Imbele  iliyotoa eneo la ardhi kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Minga, Sekondari ya Mughanga, eneo kwa ajili ya Zahanati lakini pia eneo kwa ajili ya shule mpya ya Msingi kupitia mradi wa Boost iliyopewa jina la Imbele

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Maulid Kiaratu, kwa namna ya kipekee amepongeza jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kuleta Maendeleo kwa wananchi wake kupitia miradi ya maendeleo lakini pia kwa kufungua milango kwa wahisani kuja kuunga mkono jitihada alizoanzisha za kuleta maendeleo.

Amesema katika Manispaa ya Singida , tayari wahisani kutoka Uholanzi wamejitokeza kuunga mkono jitihada za Rais  za kuleta maendeleo kwa kukarabati na  kuboresha miundombinu ya elimu katika shule ya wenye ulemavu wa kusikia katika Manispaa ya Singida.

Viongozi mbalimbali wakiweo wa Dini, Waheshimiwa madiwani, na viongozi wa chama wakiwakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Singida Mjini Bi. Lucia Mwiru aliyemwakilisha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Marther Mlata aliyepata udhuru.

Mradi wa Boost Mkoa wa Singida ulizinduliwa rasmi mwishoni mwa mwezi Aprili 2023 na Mkuu wa mkoa huo katika maadhimisho ya Sherehe za Muungano kwa kushiriki uchimbaji Msingi katika Shule Mpya ya Imbele pamoja na zoezi la upandaji miti kama sehemu ya utunzaji mazingira.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.