• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SINGIDA YATAKIWA KUMALIZA MIGOGORO YA MIPAKA BAINA YA MITAA, KATA NA WILAYA JIRANI

Posted on: September 9th, 2022

MKUU wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskasi Muragili, ametaka migogoro ya ardhi baina ya mitaa kwa mitaa na kata kwa kata katika Manispaa ya Singida ambayo ni ya muda mrefu kutatuliwa mara moja.

Mhandisi Mulagiri ametoa agizo hilo katika mkutano wa Baraza la madiwani ambapo alimwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Jeshi Lupembepamoja na timu yake kuhakikisha wanakutana na pande  zote zenye migororo na kutatua tatizo husika kwa kuwa lipo ndani ya uwezo wa Manispaa.

“hamuhitaji mtu wa nje kuja kutatua mgogoro wa mpaka baina ya mtaa na mtaa au kata kwa kata kwa kuwa ipo ndani ya uwezo wa Mkurugenzi wa Manispaa” alisema

Mkuu wa wilaya ametoa miezi miwili ya kumaliza migogoro hiyo ya ardhi na kumwelekeza Mkurugenzi na timu yake kukutana na wakurugenzi  wa wilaya za jirani zenye mgogoro wa mipaka baina yao na Manispaa ili kumaiza tatizo lililopo.

Pamoja nayo Mkuu wa Wilaya amepiga marufuku ufugaji holela wa mifugo hasa ng’ombe kwenye eneo la mji kutokana na uharibifu wa miundombinu ya barabara unaofanywa na mifugo hiyo na kusema kuwa serikali, imetumia  gharama kubwa katika ujenzi wa barabara hizo kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuzitunza.

Akizungumzia suala la mapato, Mhandisi Mulagiri aliwaagiza  waheshimiwa madiwani na wataalamu kusimamia vyema vyanzo vya mapato na kuwataka madiwani kuwa na taarifa  sahihi za mapato katika kata zao na kuvitambua vyanzo vya mapato katika maeneo yao ili waweze kuvitetea na kuvisemea katika vikao.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya, ametoa rai kwa Manispaa kuhakikisha inajenga haraka machinjio mapya katika eneo lililotengwa nje ya mji, ili kuwaondolea wananchi adha ya kupishana ovyo na ng’ombe wanaokwenda kuchinjwa katika machinjio ya zamani yaliyopo katikati ya mji wa Singida.

Katibu wa CCM Singida mjini Shaban Kalaghe amesema ni jukumu la kila mmoja kusimamia vyema maagizo ya viongozi kwa kuwayafanyia kazi na Chama kupatiwa mrejesho.

Amesema  ni jukumu la kila mmoja kuisemea miradi na jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo zinazofanywa na serikali ili wananchi wawe na ufahamu katika suala zima la maendeleo.

Akihitimisha Mkutano wa Baraza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Maulid Kiaratu aliwashukuru wajumbe kwa kumpitisha kwa sauti mmoja mgombea pekee wa nafasi ya Naibu Meya  Mh. Hassan Mkata na kumtaka kuendeleza kazi aliyokwishaianza ya kuiletea Manispaa ya Singida Maendeleo.

Mhe.Yagi alitoa agizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa  kuhakikisha anasimamia sheria, taratibu na kanuni za kiutendaji  na sheria za fedha ili kuepuka hoja za ukaguzi zisizo za msingi, kusikiliza kero za wananchi pamoja  na suala zima la usafi na mazingira pia upandaji miti.

Mstahiki Meya pia amesisitiza suala la elimu ya lishe bora ili kuondokana na utapiamlo katika Manispaa ya Singida na kumtaka Mkurugenzi kuandaa program ya mazoezi ya miili kwa watumishi na waheshimiwa madiwani.

Baraza la Madiwani jana lilimpitisha mgombea pekee wa nafasi ya Naibu Meya wa Manispaa Mh. Hassan Mkata kuwa Naibu Meya kwa kipindi cha pili. Aidha lilipitisha wenyeviti wapya wa Kamati za Kudumu za madiwani pamoja na wajumbe wa kamati hizo.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • KONGOLE MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUPEWA TUZO MAALUM YA HESHIMA NA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    May 31, 2025
  • Meya atoa onyo kwa wasiotunza mazingira Manispaa ya Singida

    May 31, 2025
  • MKURUGENZI WA MANISPAA AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI MKOA WA SINGIDA

    May 30, 2025
  • WANANCHI 35 WAFANYIWA UPASUAJI WA MTOTO WA JICHO SINGIDA

    May 29, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.