• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SINGIDA YAWEZESHA VIJANA KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Posted on: September 20th, 2022

SINGIDA,

Septemba 17, 2022.

MANISPAA ya Singida imewapatia mafunzo vijana 120, kutoka kata 18 ili kuwajengea uwezo wa kilimo cha mbogamboga,kwa njia ya teknolojia ya kitalu nyumba kwa ufadhili wa Ofisi ya Waziri mkuu,sera,Bunge,uratibu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu.

Akitoa taarifa kwa Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri mkuu, kazi, vijana na ajira, profesa Joyce Ndelichako, aliyekuwa katika manispaa ya Singida, ofisa kilimo wa manispaa ya Singida Faustine Kiyui, alisema mafunzo hayo yamegaharimu shilingi milioni 30.

“Serikali imegharamia zaidi ya shilingi milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba na mafunzo kwa vijana, waongeze uzalishaji wa mboga mboga kwa kutumia tekolojia ya kitalu nyumba….yalitolewa na wataalamu wa chuo cha kilimo Sokoine,” alisema Kiyui.

AFISA kilimo manispaa ya Singida, Faustine Kiyui (aliyesimama), akitoa maelezo juu ya mradi wa kitalu nyumba, mbele ya Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri mkuu, kazi, vijana na ajira, profesa Joyce Ndelichako, aliyefanya ziara ya siku moja kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na wizara yake.

Alifafanua kuwa, kati ya vijana hao, 20 walipata mafunzo ya ujenzi wa kitalu nyumba na wengine 100 wamenufaika na uzalishaji wa mboga mboga kibiashara, yaliyotolewa kwa nadharia na vitendo mwezi februali na machi mwaka huu ili wamudu vema kilimo hicho.

Akizungumza juu ya mradi wa kitalu nyumba, katibu wa mradi Emmaculatha Nkumbi, alisema kuwa, kutokana na mafunzo hayo, wameweza kuongeza uzalishaji, hivyo kupanua soko, kulingana na mahitaji ya mbogamboga hivi sasa.

“Naishukuru serikali kuendesha mafunzo haya kwa vijana, ni muhimu sana kwa ajili ya kuongeza kipato kwa njia ya kilimo cha kibiashara…tumekuwa shamba darasa wazuri kwa wakulima na wadau wa kilimo 150, wanaotembelea mradi,”alisema Emmaculatha.

Kutokana na mradi huo, Emmaculatha alibainisha kuwa, tangu waanze mavuno ya nyanya mwezi juni mwaka huu, zimepatikana kilo 1,420, sawa na tani 1.42, ambazo zimeingiza kiasi cha shilingi 1,420,00/=, hivyo kustawisha uchumi wa vijana.

WAZIRI wa nchi, ofisi ya Waziri mkuu, kazi, vijana na ajira, Profesa Joyce Ndelichako (wa pili kutoka kushoto), akipokea maelezo kuhusu mradi wa Kitalu nyumba, kutoka kwa katibu wa vijana, Emmaculatha Nkumbi (aliyesuka nywele), wakati Waziri huyo alipotembelea mradi huo.

KWA upande wake Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri mkuu, kazi, vijana na ajira, profesa Joyce Ndelichako, alisema mradi wa kitalu nyumba nchini unatekelezwa kwa mikoa 17, kwa zaidi ya shilingi bilioni 5.3, huku halmashauri 117, zikinufaika hadi mwaka huu.

Profesa Ndalichako alisema kuwa, kupitia mradi wa kitalu nyumba, vijana wananufaika nao kiuchumi na mpaka sasa vijana 12,000 nchini wanatekelza program hiyo muhimu kwa mustakabali mzima wa uchumi na maisha yao ya baadaye.

Alitumia fursa hiyo kumsukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kutenga fedha za kutosha, kwa ajili ya vijana, kwa kuongeza bajeti ya kilimo mara nne kwa mwaka ujao wa fedha, ikiwa ni zaidi ya mara nne, hali itayotoa fursa kwa vijana kujiajiri, kupitia kilimo.

“Kwa kweli program hii vijana wameifurahia sana na wameipokea kwa mikono miwili…namshukuru sana Rais wetu, Samia Suluhu Hassan, kuweza kutenga fedha zote hizi kwa ajili ya kuwasaidia na kuwakomboa vijana kiuchumi,”alisema Waziri.

Waziri Profesa Ndalichako alifafanua kuwa, mradi huo unawahusu vijana waliohitimu  elimu ya juu, kupitia vyuo vikuu mbalimbali, pia wale wenye kiwango cha elimu ya vyuo vya kati, kwa lengo la kuwawezesha wajiajiri kupitia sekta ya kilimo.

Wizara inategemea kuwa na miradi mingine zaidi kwa ajili ya kuwaendeleza vijana kiuchumi…. Program kwa ajil ya uwezesaji wa vijana na kuwaongezea ujuzi

 Hata hivyo Profesa Ndalichako alibainisha kuwa, kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023, serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni tisa, kwa ajili ya kutekeleza program hii muhimu na maalumu, katika maeneo yanayofuga samaki, hususani mikoa ya ziwa Victoria.


KATIBU wa vijana, kupitia mradi wa Kitalu nyumba manispaa ya Singida, Emmaculatha Nkumbi (aliyesuka nywele), akitoa maelezo ya kilimo cha mbogamboga ndani ya Kitalu nyumba, kwa Waziri Profesa Ndalichako, aliyefanya ziara ya siku moja katika manispaa ya Singida.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • KONGOLE MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUPEWA TUZO MAALUM YA HESHIMA NA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    May 31, 2025
  • Meya atoa onyo kwa wasiotunza mazingira Manispaa ya Singida

    May 31, 2025
  • MKURUGENZI WA MANISPAA AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI MKOA WA SINGIDA

    May 30, 2025
  • WANANCHI 35 WAFANYIWA UPASUAJI WA MTOTO WA JICHO SINGIDA

    May 29, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.