• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAPATO YA NDANI YANUFAISHA ZAIDI YA WATU 12,000, KATA YA MTIPA

Posted on: February 17th, 2023

WANANCHI 12,770 wa Kata ya Mtipa, katika Manispaa ya Singida, watanufaika na huduma bora za afya, baada ya ujenzi wa kituo kipya cha afya katika kata hiyo kukamilika.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe, anasema mradi huo ulitengewa Tshs. Sh. Milioni 500 kupitia mapato ya ndani, na ukikamilika utakuwa mkombozi kwa wananchi, hasa wanawake wapatao 6,300  na watoto.

Hadi kufikia Desemba 2022, Tshs. 170,187,500 zilishatumika kwa ajili ya kutekeleza mradi huo, ambao kwa awamu ya kwanza umejikita katika ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la maabara, na kichomea taka.

Jeshi amefafanua kuwa, pamoja na ujenzi kufikia katika hatua hiyo, tayari Manispaa imeshalipa fidia ya zaidi ya Tsh. 5,000,000 kwa Wananchi wane, waliotoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya.

Aidha Jeshi ameeleza baadhi ya shughuli zilizotekelezwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani kuwa ni, utoaji wa mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ambapo hadi kufikia Desemba mwaka jana (2022), vikundi 32 vimenufaika.

Shughuli zingine ni, ununuzi wa malori mawili ya kuzolea taka, ujenzi wa machinjio mpya eneo la Ng’aida na kutengeneza mtambo wa kuzolea taka, baada ya kuharibika na kuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu, bila ya kufanya kazi.

Mapato hayo pia yamegharamia ununuzi wa gari jipya aina ya Toyota Land Cruiser, kwa ajili ya shughuli za manispaa, ukarati wa miundombinu ya Kituo kikuu cha Mabasi Misuna, ambacho ni chanzo kikuu cha mapato, kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi, baada ya kununua viti 74 vya kukalia ukumbini na kwa ajili ya wakuu wa idara, na kununua madawati kwa shule ya sekondari Unyianga

Wakati huo huo Kaimu Mkurugenzi huyo, ametoa wito kwa Wanachi hakikisha wanalipa tozo, ushuru na leseni kwa wakati, ili kuiwezesha Manispaa kutoa huduma bora kwa wananchi wake kwa wakati.

Manispaa ya Singida ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 23,  vikiwemo 12 vya serikali na 11 vya sekta binafsi, huku Ujenzi unaoendelea katika mradi wa Kituo cha Afya Mtipa, hadi sasa umetoa ajira 20 kwa vijana, na wanawake watano.

.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.