• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MIAKA MIWILI YA DHAHABU YA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN YALETA MAPINDUZI YA MAENDELEO SINGIDA

Posted on: March 18th, 2023

Serikali imeongeza fedha za miradi ya maendeleo na utawala Mkoani Singida, kutoka Sh.Bilioni 180.18, mwaka 2020/21, hadi kufikia Sh. Bilioni 239.8 mwaka fedha 2022/2023, sawa na asilimia 33.09.

Akieleza mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amesema fedha hizo zimeleta mageuzi makubwa katika sekta ya elimu, afya na maji, barabara na kufungua milango ya uwekezaji kwa wawekezaji wanaotoka nje,ili kuwekeza mkoani hapa.

“Mafanikio ya serikali ya awamu ya sita ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025…mkoani Singida imeleta mageuzi makubwa, ikiwemo mwekezaji wa kilimo cha alizeti na mgodi wa Shanta kule Ikungi, takaofunguliwa hivi karibuni,”alisema.

Amesema kuwa, ongezeko hilo la bajeti, limeboresha huduma za kijamii na kiuchumi, katika mkoa wa Singida, hususani mradi wa ujenzi wa vituo vya afya kwa kata 20, zahanati 51 na hospitali mpya nne za wilaya za Mkalama, Ikungi, Singida vijijini na Itigi.

“Mkoa ulipokea Sh. 6,650,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya nne za wilaya, Sh. 8,900,187,500/= za ujenzi wa vituo vya afya 20 na 2,550,000,000/= kukamilisha zahanati 51, zilizojengwa na wananchi huko vijijini,”alibainisha Serukamba.

Serukamba amefafanua zaidi kuwa katika  kipindi hiki cha miaka miwili Mkoa umepokea Sh. 11,833,184,333/30 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya hospitali ya mkoa, kwa ajili ya jengo la wagonjwa mahututi, jengo la dharula, nyumba za watumishi na ununuzi wa vifaa tiba.

Pia fedha hizo zilitumika kukarabati vyumba vya CT-SCAN na DIGITAL X-Ray, ujenzi wa jingo tengefu la sakafu 4 (Covid-10 containment center) na mafunzo kwa watumishi juu ya huduma za EMD, ICU na CT Scan.

Licha ya mafanikio hayo ya afya, Serukamba ameeleza mafanikio mbalimbali, katika sekta ya elimu, maji na miundombinu kadhaa, ikiwemo barabara.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Jeshi Godfrey Lupembe, amesema kuwa, katika kipindi cha 2021/22- 2022/23 Halmashauri ya Manispaa ya Singida ilipokea ruzuku kutoka serikali kuu kiasi cha Tsh. 6,461,700,614 kwa ajili ya miradi ya maendeleo wakati  kiasi cha Tsh. 1,130,227,683 kilichotokana na mapato ya ndani kimeelekezwa katika miradi ya maendeleo.

Amesema katika kipindi hicho, Manispaa imetoa mikopo ya zaidi ya Sh. Milioni 400/= kwa ajili ya vikundi mbalimbali ikiwa ni azma ya serikali ya kuwezesha sekta zisizorasmi kupitia vikundi vya wajasiariamali ili kujiendesha na kukuza uchumi wa taifa.

Kwa mujibu wa Jeshi, vikundi hivyo ni vile vya ujasiriamali kwa wanawake, vijana na kundi maalumu la wenye ulemavu zaidi ya 77, kupitia fedha za mapato ya ndani (10%).

Aidha, Lipembe amesema licha ya kutoa mikopo,Halmashauri ya Manispaa  imefanikisha ujenzi wa vituo vya afya 04, ukamilishaji wa ujenzi wa zahanati 06 na kujenga jengo la mama na mtoto kwenye vituo viwili  vya afya Sokoine na Mtisi kupitia fedha za serikali kuu na zile zilizotokana na mapato ya ndani.

Jeshi amesema licha ya sekta ya Afya,  lakini pia serikali imeboresha miundombinu ya shule za msingi na sekondari kwa kujenga vyumba 50 vya madarasa ya shule za sekondari, ujenzi wa shule mpya  moja ya sekondari ya kata ya Uhamaka, ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule za msingi na shule shikizi, ujenzi wa jengo la Utawala la Manispaa ambapo shilingi bilioni moja zimepokelewa kwa ajili ya mradi huo na ununuzi wa magari 02 ya ubebaji taka kwa fedha za mapato ya ndani.

Jeshi amefafanua zaidi ya kaya 2,473 zimenufaika kupitia program ya kunusuru kaya maskini ambapo malipo ya ruzuku ya msingi na utimizaji masharti ya Afya na Elimu kupitia TASAF  kiasi cha 1,511,748,000 yamefanyika.

Matangazo

  • MAPITIO YA BAJETI 2022/2023 February 21, 2023
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA MANISPAA YA SINGIDA KWA SHULE 2021 November 15, 2021
  • KARIBU UWEKEZE KATIKA MANISPAA YA SINGIDA November 15, 2022
  • TATHMINI YA MATOKEO YA MITIHANI YA DARASA LA SABA 2022 KI- SHULE December 23, 2022
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • KAYA 5,396 MANISPAA YA SINGIDA ZIMENUFAIKA NA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF) DIRISHA LA SEPTEMBA - OKTOBA, 2023

    March 22, 2023
  • BOT YATOA ELIMU YA FEDHA BANDIA KWA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA KIMATAIFA LA VITUNGUU, MISUNA MANISPAA YA SINGIDA

    March 20, 2023
  • TUME YA UTUMISHI YA WALIMU SINGIDA YAWATAKA WALIMU KUZINGATIA SHERIA,KANUNI NA MIONGOZO INAYOTOLEWA NA SERIKALI

    March 20, 2023
  • MIAKA MIWILI YA DHAHABU YA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN YALETA MAPINDUZI YA MAENDELEO SINGIDA

    March 18, 2023
  • Tazama Zote

Video

Waziri Jafo atoa maagizo mazito kwa ma-RAS, ma-DED, Wakuu wa idara na maasifa mawasiliano serikalini
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.