• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKOA WA SINGIDA WAZINDUA WIKI YA UPANDAJI MITI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA

Posted on: January 29th, 2022


Mkoa wa Singida leo tare 29 Januari, 2022 umezindua wiki ya upandaji miti ambapo miche ya miti 2000 imepandwa kandokando ya fukwe za Ziwa kindai na Munangi katika Manispaa ya Singida.

Akizindua zoezi la upandaji miti, Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Binilith Mahenge, alisema lengo la upandaji miti ni katika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi lakini pia kupendezesha mandhari mkoa na kuufanya kuwa wa kuvutia.

“sote tumeshuhudia mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyopelekea kuchelewa kwa mvua, hivyo kwa kupanda mti kutasaidia kukabiliana na changamoto hizo pia kuleta mandhari nzuri katka mkoa wetu” alisema.

Mkuu wa Wilaya aliwataka wananchi kujenga tabia ya kutunza mazingira na usafi bila kusubiri siku maalum iliyotengwa kwa shughuli hiyo kuanzia kwenye ngazi ya kaya kwa kuhakikisha mazingira yanakuwa salama na safi wakati wote.

Aidha amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Ndg. Zefrin Lubuva kuelekeza Vijana wake kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wote wanaotumia vibaya vizimba vya taka kwa kutupa taka nje ya vizimba hali inayochafua zaidi Mazingira.

“Kuna baadhi ya watu hutumia vibaya vizimba vya taka badala ya kutupa taka ndani ya kizimba hutupa nje hivyo namwagiza Mkurugenzi kuweka utaratibu maalum kupitia vijana wake kukamata wale wanaotupa taka nje na kuwachukulia hatua” alisisitiza Mkuu wa Wilaya

Mkuu huyo alitoa agizo kwa Mkurugenzi kwa Manispaa kupitia Viongozi wa Serikali za mitaa kuhakikisha kila kaya inapanda miti 2 na   kufanya ukaguzi kwa kila nyumba na kaya zitakazokaidi kupanda miti  kuchukuliwa hatua na kuongeza kuwa kwa maeneo yaliyo nje ya mji kila kaya inapaswa kupanda miti isiyopunua 5.

Mhandisi Mulagiri pia amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa kuhakikisha sheria ndogo za uhifadhi mazingira zinasimamiwa vyema ili kuepuka uharibifu wa Mazingira hasa unaosababishwa na uchungaji holela wa mifugo.

Naye Afisa Mazingira wa Manispaa ya Singida Bi. Shuku Kaishwa akisoma taarifa kuhusiana na Mazingira alisema  upandaji miti ni zoezi endelevu kwani  uwepo wa miti ya kutosha kunasaida kuhifadhi hewa ya ukaa na hivyo kupunguza madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwa ni pamoja na kusababisha mmomonyo  wa ardhi na kukauka kwa vyanzo  vyanzo vya maji.

Bi. Shuku aliendelea kubainisha kuwa katika kufanikisha lengo la kitaifa la kupanda miti 1,500, Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wakala wa Misitu (TFS), Tree for Future Pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya imeanza zoezi la ugawaji miti kwa taasisi mbalimbali na watu binafsi ambapo hadi sasa jumla ya miche ya miti 100,000 imegawiwa. Zoezi hili linaendelea.

Aliendelea kusema kuwa Halmashauri ya Manispaa katika kukabiliana na changamoto za kimazingira imejipanga kwa kuhakikisha kila taasisi inapewa eneo la kudumu la kupanda miti,  kuitunza miti iliyopandwa msimu huu wa mvua ili kupata matokeo chanya, kuhamasisha Jamii na taasisi kuanzisha mashamba ya miti na kuendelea kutoa elimu kwa Jamii kutokata miti yote wakati wa uandaaji mashamba.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MEI MOSI - MAJALIWA

    April 30, 2025
  • KIKWETE AFUNGA MICHEZO UWANJA WA CCM LITI

    April 30, 2025
  • "UMUHIMU WA MFUMO BORA WA USALAMA WA AFYA KAZINI"

    April 28, 2025
  • "UMUHIMU WA MFUMO BORA WA USALAMA WA AFYA KAZINI"

    April 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.