• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKURUGENZI WA SINGIDA AWAPONGEZA VIONGOZI WAPYA WA SERIKALI ZA MITAA

Posted on: November 28th, 2024


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Bi. Joanfaith Kataraia, amewapongeza viongozi wapya wa Serikali za Mitaa na kuwaasa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kusimamia mapato, miradi ya maendeleo, na kuwa sauti ya wananchi kwa kusikiliza kero zao.


Kauli hiyo imetolewa leo, Novemba 28, 2024, wakati viongozi wapya wa Serikali za Mitaa kutoka Kata zote walioshinda kula kiapo katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo (FDC), Manispaa ya Singida.

Viongozi hawa ni pamoja na wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji, pamoja na wajumbe mchanganyiko na wajumbe wanawake, ambao walipigiwa kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024, kote nchini.


Bi. Kataraia aliwapongeza viongozi hao na kuwaasa kuzingatia majukumu yao muhimu katika utawala wa Serikali za Mitaa.

Alisisitiza kwamba viongozi hawa wanapaswa kuhakikisha mikutano ya kijamii inafanyika, kutekeleza miradi ya maendeleo, kusimamia mapato na matumizi, pamoja na kutatua migogoro mbalimbali, ikiwemo migogoro ya ardhi.


“Mtakuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na mapato yanakusanywa na kutumika kwa manufaa ya wananchi. Lakini, ni muhimu kuhakikisha usalama na amani katika maeneo yenu, na kusimamia masuala ya afya, elimu, mazingira na usafi,” alisema Bi. Kataraia.


Pia, aliwakumbusha viongozi hao kuwa uchaguzi umemalizika, na kwamba ni wakati wa kuwahudumia wananchi bila kujali tofauti za kisiasa, kidini, au kijamii. Alisisitiza umuhimu wa viongozi hao kuwa mfano bora kwa jamii, kwa kuhakikisha demokrasia inajengwa na wananchi wanaunganishwa katika maendeleo.


“Tunawategemea nyinyi kuwa viongozi wa mfano, kuhakikisha kwamba mnafanya kazi kwa bidii na kwa manufaa ya wananchi wote. Msiache kumsaidia Mh. Rais (Dkt Samia Suluhu Hassan) na kuwaunga mkono wananchi katika juhudi za maendeleo,” alisisitiza Bi. Kataraia.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.