• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKUU WA MKOA AISHAURI MANISPAA KUANDAA MIKAKATI ITAKAYOIMARISHA USAFI WA MJI WA SINGIDA

Posted on: January 20th, 2023

Halmashauri ya Manispaa ya Singida imeshauriwa kuandaa mikakati itakayoimarisha usafi wa mji, sambamba na ukusanyaji wa ada za taka, inakayotozwa kwa kila mwezi Sh. 2,000.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, ametoa rai hiyo kwenye ziara ya siku moja, katika Manispaa ya Singida, wakati akikagua hali ya usafi na uzoaji wa taka, kwenye vizimba.

Serukamba amesema kuwa, Halmashauri ya Manispaa ya Singida, inalo jukumu kubwa kuhakikisha hali ya usafi inaimarika, ili kuondoa kero na hatari ya mji huo kupatwa na maradhi ya mlipuko.

“Hali ya usafi ya mji hairidhishi, hasa maeneo ya vizimba…hakikisheni mnadhibiti tatizo hili la taka, ili kuepuka magonjwa ya mlipuko,” alisema Serukamba.

Kadhalika Serukamba, ameitaka Manispaa ya Singida, kuandaa mkakati madhubuti utakaowezesha kila kaya kuchangia ipasavyo gharama za uzoaji taka, ili kuuwezesha mji kuwa safi.

“Tubadilike, umefika wakati kila mtu anazalisha taka lakini hachangii gharama ya kuziondoa…ni jukumu la kila mmoja kushiriki katika usafi kwa kuchangia gharama”, amesisitiza Serukamba

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa amemwagiza Kaimu  Mkurugenzi wa Manispaa, Jeshi Lupembe, kuhakikisha maeneo yote ya wazi, ambayo yanatumika kwa ajili ya kukusanyia taka (collection point) yanasafishwa na kupandwa miti ili kuboresha mazingira ya mji .

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskasi Muragili, amesema zoezi la usafi wa mji ni shirikishi, kati ya Watumishi wa sekta zote na wananchi kwa ujumla, kwa lengo la kuuweka mji wa Singida katika hali ya usafi.

“ Kila mmoja wetu kwa nafasi yake awajibike sana katika kuhakikisha Mji unakuwa safi…Watendaji wa Mitaa na Kata, mshrikiane kusimamia zoezi hili, kwenye maeneo yenu,” amesisitiza Muragili.

Pia Mkuu huyo wa Wilaya, ametumia fursa hiyo kuhimiza upandaji miti kwenye Kata na maeneo ambayo bado yako nyuma, katika kutekeleza zoezi hili na kuwataka Watendaji kuhakikisha wanafikia lengo la upandaji miti, ifikapo 30, Januari, 2023.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Maulid Kiaratu, amewataka walezi wa Kata, kushirikiana vyema na Watendaji wa Kata wanazozilea, ili kufikia malengo ya ukusanyaji mapato na hasa ada za uzoaji wa taka, kwa asilimia kubwa

Kupitia ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Jeshi Lupembe, alimshukuru Mkuu wa Mkoa, na akaahidi kusimamia vyema maelekezo yote aliyoagiza, ya usafi wa mji na ukusanyaji mapato.

Amesema kuwa, changamoto kubwa inayoikabili Manispaa ni uhaba wa magari ya uzoaji wa taka, pamoja na ubovu wa mtambo wa kuzoa taka.

Lupembe, amefafanua kuwa, ili kupunguza gharama ya uzoaji wa taka kutokana na gharama kubwa ya kukodi magari, Manispaa imejiwekea mkakati wa kununua malori mawili, kwa ajili ya kurahisisha kazi hiyo.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.