• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

NAIBU MEYA: SIMAMIENI VYEMA FEDHA ZA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA

Posted on: November 26th, 2022

Naibu Meya wa Manispaa ya Singida, Hassan Mkata, amewataka Madiwani na viongozi wengine wa Umma, kusimamia vema fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa, ili yaweze kutumiwa na wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza, ifikapo Januari mwakani (2023).

Naibu Meya huyo amesema hayo kwenye Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani, uliofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwenge mjini Singida, pamoja na mambo mengine kupokea taarifa ya robo ya kwanza ya mwaka, kwa ajili ya utekelezaji miradi ya maendeleo.

Amesema, Manispaa ya Singida imepokea fedha za ujenzi wa vyumba hamsini vya madarasa ya shule za Sekondari, na yanatakiwa kukamilika ifikapo desemba 15 Mwaka huu, hivyo ni jukumu lao wote kushirikiana ili kukamilisha kazi hiyo.

”Kutokana na Serikali kutupatia fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza januari mwakani, sote tuna wajibu wa kusimamia kwa karibu, ili yakamilike kwa wakati,” alisema Naibu Meya.

Aidha katika hatua nyingine Madiwani hao wamemwomba Wakala wa Barabara, Mijini na Vijijini (TARURA), kuongeza bidii ya kutengenza, kufungua na kukarabati barabara kwenye maeneo mbalimbali ya Manispaa, ili kumaliza kero kwa jamii, hususani kuelekea kipindi  hiki cha mvua za masika.

Baadhi ya Madiwani hao akiwemo, Kawawa Munjoli, Hamisi Kinyeto na Ibrahim Murua, na Magreth Malecela pamoja na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na TARURA, lakini wametaka umakini zaidi katika matengenzo, pia itanue wigo wa shughuli zake, lengo likiwa ni kuwezesha barabara zote kupitika wote.

Meneja wa TARURA Wilaya ya Singida, Mhandisi Lambert Bayona, amesema mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga zaidi ya Sh. Bilioni 2.25, kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za matengenezo ya barabara, katika Manispaa ya Singida.

Mhandisi Bayona amefafanua kuwa kati ya fedha hizo, Sh. Milioni 500/- zimetokana na Tozo, zaidi ya Sh. Bilioni 1.25/- zitatoka kwenye Mfuko wa Barabara na fedha zingine Sh. Milioni 500/-, zikiwa ni fedha za kila Jimbo.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Jeshi Lupembe, akijibu maswali ya papo kwa papo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa robo ya kwanza.


Mwenye kiti wa Chama cha Mapinduzi , Lucia Mwiru, akizungumza kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa robo ya kwanza

Wajumbe wa Baraza la Madiwani wakiwa wamesimama tayari kwa ajili ya dua kabla ya Mkutano wa Baraza la Madiwani wa robo ya kwanza kufunguliwa

Waheshimiwa madiwani  Hamis Kisuke ( Misuna), Emanuel Emadaki (Mwankoko) na Ibrahimu Mruwa (Minga) wakichangia hoja baada ya mawasilisho ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo za  taasisi za Umma zikiwemo TARURA, SUASA na TANESCO kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya kwanza


Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.