• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

OSCAR MWAKALOBO: MUUGUZI, MWELIMISHAJI JAMII NA MSIMAMIZI WA MRADI, ATWAA TUZO YA MWEZI

Posted on: November 16th, 2022

Manispaa ya Singida imeendelea kuhamasisha utendaji kazi sehemu  za kazi ili kuweza  kupata matokeo chanya yatakayoinufaisha  serikali katika mipango yake ya maendeleo.

Hali hii imetokana na utaratibu ulioanzishwa na Manispaa ya Singida, wa kushindanisha watumishi kwenye idara na vitengo vyake vyote, kwa lengo la kuleta tija na ufanisi katika eneo la kazi.

Akizungumza kwenye hafla ya kumtangaza mtumishi Hodari wa mwezi Oktoba Bw. Oscar Laiton Mwakalobo, Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Manispaa ya Singida, Kulanga Matiya Kanyanga, amesema  Mchakato huo ni moja ya mikakakati iliyobuniwa kwa lengo la kuamsha ari ya utendaji kazi kwa watumishi.

Amesema kuwa, jambo la kuwamotisha watumishi linajenga uhusiano mwema, ushirikiano, kujiamnini na kuaminiwa  kati ya mwajiri na mwajiriwa, hivyo kuiwezesha Manispaa kufikia malengo yake, ya maendeleo kwa jamii

Kulanga amefafanua kuwa, zoezi hilo limeboreshwa baada ya kupokea maoni kutoka kwa wadau na ofisi kuyafanyia kazi, ikiwemo kuunda timu ya watu nane inayojumuisha wakuu wa idara wachache, baadhi ya watumishi na viongozi wa vyama vya wafanyakazi.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Aristideus Mulokozi, ametumia fursa hiyo kumpongeza mtumishi Hodari kwa mwezi Oktoba, na akatoa rai kwa watumishi wengine kufanya kazi kwa biddi na weledi ili kuiletea maendeleo Manispaa.

Kupitia fursa hiyo, Mulokozi amemwagiza Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala, kuboresha kifungu cha motisha, wakati wa mapitio, ya nusu mwaka ya bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023, hali itakayoongeza gthamani ya utumishi.

“ Pamoja na pongezi hizi, nimwagize mkuu wa idara ya utumishi na utawala, ahakikishe kipindi cha budget review, anaboresha kifungu cha motisha ili mtumishi Hodari wa kila mwezi aweze kupewa zawadi bora, itakayoongeza thamani ya utumishi wake,” amesema Mulokozi.

Kwa upande wake Kaimu Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) mkoa wa Singida Bi. Juliana Muhinjo, amesema uongozi wa chama unaipongeza Manispaa kwa ubunifu huo, ambao unajenga ari ya uwajibikaji.

Amesema kuwa, TALGWU, itakuwa bega kwa bega katika kutekeleza mpango huo, huku akihidi kukamilisha taratibu za kuzawadia watumishi hodari, kwa ajili ya kuunga mkono zoezi hilo linalotekelezwa na Manispaa ya Singida.

Kaimu mganga mkuu wa Manispaa Dk.Hamisi Juma Yuna, amesema mtumishi Hodari wa mwezi Oktoba, anayetoka katika idara ya afya Bw. Oscar Mwakalobo, ameshinda kwa haki, kutokana na juhudi binafsi katika kuitumikia jamii.

Amesema kuwa, Mwakalobo ni Muuguzi, lakini pia analo jukumu la kusimamia mradi wa ujenzi wa majengo ya mama na mtoto na lile la upasuaji, kazi aliyoifanya vizuri, na kuwaridhisha wakaguzi wa mradi wanaofika kituoni hapo.

“ Oscar ni muuguzi kwa taaluma, hajawahi kuwa mhandisi wala mtunza hesabu, lakini amesimamia mradi wa jengo la mama na mtoto na lile la upasuaji, huku pia akitekelezwa majukumu yake ya uuguzi kwa ufanisi”, amesema Dk. Yuna.

Akiushukuru Uongozi wa Manispaa, Mwakalobo, ameahidi kuongeza juhudi zaidi kazini, ili kulinda heshima na tuzo aliyoipata, kwa lengo la kuiletea maendeleo jamii ya kata ya Mtamaa, Manispaa ya Singida na Taifa kwa ujumla.

Amewataka watumishi wengine kujituma kazini bila kujali nafasi zao “ Mimi ni muuguzi, lakini nasimamia pia mradi wa ujenzi  na naelimisha jamii kwa ajili ya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF, ambao kwa mwezi Oktoba, nimeweza kufikisha asilimia 60% ya uandikishaji,” ameeleza Mwakalobo

Halmashauri ya Manispaa ya Singida imeazisha programu ya kuwamotisha watumishi hodari kila mwezi katika mwaka wa fedha 2022/2023, huku mshindi wa kwanza katika program hiyo akiwa Bi. Bahati Samwaja kwa mwezi Septemba, ikihusisha jumla ya watumishi 1,546, waliopo sasa.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.