• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC DENDEGO AWAPONGEZA MADIWANI MANISPAA YA SINGIDA ATAKA HALMASHAURI KUWA YA MFANO

Posted on: June 14th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, amewapongeza Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa kazi nzuri wanayoifanya licha ya changamoto chache zilizopo, huku akiwataka wataalamu kuhakikisha hoja za ukaguzi hazizidi katika halmashauri hiyo.


Mhe. Dendego alitoa pongezi hizo leo Juni 14, 2025, wakati wa Baraza la Kujadili Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), lililofanyika katika Ukumbi wa Polisi Makao Makuu, Manispaa ya Singida. Baraza hilo lililenga kupitia, kupima mapato na matumizi ya fedha pamoja na utendaji wa halmashauri kwa ujumla.


Katika taarifa ya CAG, Manispaa ya Singida ilipata hati safi na kubakiwa na hoja 17, ambapo tano kati ya hizo ni za kisera na 12 zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.


Akizungumza kwenye baraza hilo, Mhe. Dendego alisema kuwa licha ya changamoto zilizopo, madiwani wamekuwa wakitimiza majukumu yao ipasavyo katika kata zao na wanastahili pongezi kwa kujituma na kuonyesha uongozi makini.


“Changamoto zipo na hazitishi, ila Waheshimiwa Madiwani mko vizuri. Mnahitaji sehemu ndogo tu kumalizia, na mkimalizia hiyo basi Halmashauri ya Singida itaendelea kung’ara kama halmashauri nyingine nchini,” alisema Dendego.


Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza kuwa hapendi kuona halmashauri inakuwa na hoja nyingi za ukaguzi, akiwataka viongozi na watendaji wa Manispaa hiyo kuwa mfano wa kuigwa katika halmashauri za mkoa huu, kwa kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kwa kuzingatia sheria.


Matangazo

  • NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA SINGIDA June 03, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • VIKUNDI 55 VYAPATIWA MAFUNZO KABLA YA KUPOKEA MIKOPO YA 10%

    June 29, 2025
  • SINGIDA MANISPAA YAANZA KUTOA ELIMU YA UCHAGUZI MKUU KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • USAFI WA NGUVU KUELEKEA MWENGE WA UHURU

    June 28, 2025
  • UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA WAFIKIA ASILIMIA 80

    June 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.