• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SINGIDA: SIMAMIENI VIZURI VYANZO VYA MAPATO ILI KUPUNGUZA HOJA ZA UKAGUZI

Posted on: June 15th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Binirith Mahenge ameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Singida kuhakikisha inasimamia vyema kazi ya ukusanyaji mapato na kwamba kazi hiyo haina mjadala hivyo kutumia mamlaka yake kuhakikisha mapato yanakusanywa ipasavyo.

RC Mahenge ameyasema hayo leo (tarehe15.06.2022) katika kikao cha Baraza maalum la madiwani la kujadili hoja za ukaguzi za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) ambapo jumla ya hoja 68 ziliibuliwa, 51 kati ya hizo zilifungwa na hoja 17 zilijadiliwa na kuridhiwa majibu yake. Hoja hizo ni kwa mwaka 2020/2021 na mwaka kaguliwa 2021/2022.

Dr. Mahenge alisema mapato yakikusanywa vizuri hoja zitapungua kwani miradi mingi itapelekewa fedha na hivyo kukamilishwa kwa wakati. Aidha amemtaka Mkurugenzi na timu ya menejimeti kufanya tahmini ya kila chanzo ili kubaini mapungufu katika ukusanyaji wa mapato na hivyo kuboresha kwa kuwa na usimamizi mzuri wa vyanzo hivyo.

“ pongezi zangu nyingi kwa Mstahiki Meya kwa usimamizi mzuri wa Halmashauri na kupelekea kupata hati safi mwaka 2020/2021 pia kwa Baraza lake la madiwani kwa kuwa na hoja chache ukilinganisha na mabaraza mengine niliyopita” alisema Dr. Mahenge

Amewataka wajumbe wa Baraza hilo kutambua umuhimu wa Manispaa pia nafasi yake katika Mkoa na kuwataka madiwani na wataalamu kuendelea kushirikiana katika a kusimamia ukusanyaji wa mapato ili kuijenga Manispaa ya Singida ambayo ndiyo uso wa Mkoa wa Singida.

Pamoja na masuala ya mapato Mkuu wa Mkoa alipongeza juhudi zinazofanywa na Manispaa ya Singida ya kuuweka mji katika hali ya usafi kwa kumpata mzabuni wa usafi na kusisitiza kuwa usimamizi uendelee na mzabuni ahimizwe kupita maeneo yote na atumie magari imara.

“Tusiwakatishe tamaa wananchi kwa kushindwa kuwawekea mazingira safi na salama wakati tunachukuwa ada ya taka na ushuru mbalimbali” amesisitiza.

Dr. mahenge ametumia wasaa huo pia kuhimiza suala la umuhimu wa kutenga eneo la maegesho la magari kama chanzo cha mapato lakini pia kuweka ustarabu na usalama wa magari badala ya kuacha uegeshaji holela wa magari.

Aidha amesisitiza Halmashauri kuhakikisha imepima eneo la uwekezaji na kwamba wawekezaji watakaojitokeza wapatiwe eneo kwa masharti nafuu. Pamoja nayo ameshauri vivutio vya utalii hasa fukwe za maziwa Kindai na Singidani ziendelezwe kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni za uhifadhi wa Mazingira.

Mkuu huyo wa mkoa amewapongeza wataalamu wa Manispaa kwa kazi nzuri iliyofanyika katika zoezi la anwani za makazi na kutaka ushirikiano uliowezesha zoezi hilo uendelee katika utekelezaji wa majumu mengine hasa ya ukusanyaji mapato.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Mulagiri almetoa pongezi kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu kwa kazi nzuri iliyofanywa na wataalamu wa Manispaa ambayo ni ishara ya ushirikiano mwema.

“Endeleeni kuwa na moyo huo huo wa kufanya kazi kama timu ili kuleta matokeo chanya” amesema Mkuu wa wilaya.

Mstahiki Meya Mhe. Yagi Kiaratu amezungumzia hoja zilizojitokeza ambazo zimejadiliwa na baraza hilo na kusema ni wajibu wa wajumbe wa baraza hilo kwa kushirikiana na wataalamu kuhakikisha marejesho ya mikopo ya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu inarejeshwa kwa wakati ili kuepuka hoja kama hizo kujirudia.

Aidha amesema ni wajibu sote kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati kwani ni aibu kwa Halmashauri ya Manispaa kushindwa kukamilisha miradi wakati rasilimali zipo na wasimamizi wapo.

“Ni aibu kushindwa kukamilisha miradi hiyetu kwa wakati wakati miradi kama hiyo katika Halmashauri nyingine inakamilika” alisisitiza Mhe. Yagi

Mhe. Yagi alimpongeza Mkuu wa Mkoa Dr. Mahenge kwa maono yake ya kuzitaka Halmashauri kupitia hoja za ukaguzi kila mwezi hali iliyorahisisha kazi ya ujibuji wa hoja kwa ufanisi na kwa wakati na hivyo kupelekea hoja nyingi kufungwa.

Pamoja na hoja hizo Mstahiki Meya Mhe. Yagi amepongeza bajeti ya Serikali iliyopitishwa jana (14/06/2022) na kusema ni bajeti iliyomuangalia zaidi mwananchi na kwamba kwa bajeti hiyo wananchi wategemee mazuri  mengi katika mustakabali mzima wa Maendeleo yao na ya  taifa kwa ujumla.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.