• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI ITAENDELEA KUTOA MATIBABU BURE KWA WAZEE

Posted on: October 5th, 2021

Serikali itaendelea kusimamia utoaji wa matibabu kwa Wazee bila malipo, upatikanaji wa dawa Hospitalini  na uwepo wa dirisha maalum kwa ajili ya Wazee ili kuwaenzi na kuwaondolea usumbufu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa  wilaya ya Singida Mjini Mhandisi Paskasi Muragili kwaniaba ya Mkuu wa mkoa wa Singida wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wazee Duniani yaliyofanyika mjini Singida.

 Amesema Serikali itaendelea kutoa huduma kwa wazee pasipo kuchangia gharama za matibabu na kuboresha changamoto ambazo zimejitokeza katika utoaji wa huduma hiyo kwa kundi hilo.

 "Sisi sote ni mashahidi wa utolewaji wa huduma za Afya bila malipo kwa Wazee wote. Nitoe wito kwenu kufika kwenye vituo vya huduma za Afya vya Serikali ili kupatiwa huduma bila kuchangia gharama za matibabu".

Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewaagiza Wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani humo kuendelea kuwachangia wazee wasio na uwezo na kuwaunganisha kwenye Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (iCHF) na wale wenye uwezo wa kujiunga wenyewe amewahamasisha wajiunge ili kuendelea kuboresha huduma za Afya.

Awali Mwenyekiti wa umoja wa Wazee hao SAWATA Bw. Ramadhani Juma Moghu ameishukuru Serikali kwa hatua walizoendelea kuzichukua katika kuimarisha Sekta hasa kwa wazee.

Akijibu hotuba ya wazee hao Mkuu huyo wa wilaya amewataka Maafisa maendeleo ya jamii wa kila Halmashauri kuwashauri wazazi  ambao watoto wao wanaolelewa na wazee kuona umuhimu wa mtoto kuishi na mzazi ili  kuwapunguzia majukumu.

Amesema Wazee wengi wameachiwa watoto na watoto wao au wajukuu. Malezi ya watoto hao ni jukumu la wazazi wao hivyo ni vema tukawaelimisha watoto na wajukuu zetu juu ya umuhimu wa malezi ya Wazazi kwa watoto. Alisistiza Muragili

 "Kwa kuwa kila Halmashauri kuna Ofisi za Ustawi wa Jamii niwaombe mfike ili wazazi hawa waweze kuwajibika kama Sheria ya Mtoto Na. 21 ya Mwaka 2009 inavyoelekeza".

“Nitoe shukrani kwa viongozi wa Baraza la Wazee mkoa na Viongozi wa SAWATA katika kufanya maandalizi na kufanikisha maadhimisho haya.  Aidha, nazishukuru Taasisi zote zilizoweza kutoa michango yao ya hali na mali katika kuwezesha maadhimisho haya”.  Alimalizia Muragili.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.