• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI YAAHIDI KUWASAIDIA WALEMAVU KUPATA ELIMU BORA

Posted on: February 22nd, 2024

SERIKALI imesema itaendelea kutoa sapoti kubwa kwa watu wenye ulemavu kuhakikisha wanapata elimu na vifaa saidizi ambavyo vitahitajika.

Hayo yamesemwa leo Februari 22, 2024 na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya, Dkt. Wilson Mahera katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Maandishi ya Braille (walemavu wasioona) ambayo yamefanyika Mkoani Singida, katika Halmashuri ya Manispaa Singida.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Braille kwa mwaka huu inasema 'Eneza Ufahamu umuhimu Braille'.

Katika maadhimisho hayo, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imepanga kuhakikisha inaendelea kutoa sapoti ya elimu na vifaa saidizi kwa wote wenye changamoto ya Braille kuanzia hatua ya awali.

Dkt. Mahera alieleza kuwa, Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuhakikisha elimu na vifaa saidizi vinawafikia walengwa wote.

"Katika eneo la elimu kwa walemavu (wasioona) kwa mwaka 2022-23 tumefanikiwa kuwaandikisha wanafunzi wa awali wapatao 2873, wasichana 1328 na wavulana1545, kwa upande wa shule ya msingi wanafunzi 3685 waliandikishwa, wasichana 1768 na wavulana 2217.

"Elimu ya Sekondari waliandikishwa wanafunzi 1784, wasichana 837, wavulana 947, lakini kuna wale MMEKWA waliandikishwa 243, wasichana 120 na wavulana 123.

"Lakini katika kuboresha elimu kwao, Serikali imejenga mabweni 50 katika Halmashuri 50 na hii inathibitisha nia njema ya serikali ya awamu ya sita katika kuhudumia watu wenye ulemavu.

"Serikali inawashirikisha vyema wadau ambapo kwa pamoja wanaendesha kampeni ya kutoa huduma saidizi mashuleni kwa watoto wa kike kama kutoa taulo za kike, kampeni hizi zinaunga mkono Serikali katika upatikanaji wa mahitaji ya watoto wenye ulemavu," alisema Dkt. Mahera.

Aidha Dkt Mahera alisisitiza kuwa Serikali imeendelea kushirikiana na wadau kwa kutoa vifaa.

"Serikali kwa kushirikiana na wadau inaendelea kutoa vifaa saidizi kwa kutumia bajeti yake yenyewe na kushirikiana na wadau kama ambavyo mmeona leo hapa.

"Lakini kupitia fedha za mkopo kutoka kwa Shirika la Fedha Duniani, Serikali imetumia kiasi cha milioni 770 kununua vifaa saidi kwa ajili ya walemavu kama Bajaj, Shime Sikio, vifaa vya kukuzia usikivu, kompyuta mpakato na vishikwambi.

"Serikali na wadau wake kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Ulemavu imetoa fimbo nyeupe 35, mafuta kinga 35, viti mwendo 35," alibainisha Dkt. Mahera.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasioona Tanzania, Omary Itambu, amemshukuru Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sapoti kubwa ambayo amekuwa akitoa kwa upande wao.

Kiongozi huyo amefunguka kuwa: "Serikali hii imekuwa ikitupa sapoti hasa mama yetu (Rais), mfano TAMISEMI iligawa vishikwambi kwa walimu, lakini haikubagua, walimu wasioona wote walipata na ninaamini mambo mazuri yanakuja.

"Rais amefanya makubwa sana kwetu hasa kwa upande wa elimu na sasa tunamuomba aongeze nguvu kwenye suala la afya."

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.