• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TARURA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA YAWASILISHA MPANGO NA BAJETI WA MIAKA MINNE 2022/2023 - 2025/206

Posted on: January 5th, 2022


Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida imewasilisha Mpango na Bajeti kwa kipindi cha miaka minne (4) kuanzia 2022/2023 hadi 2025/2026 utakaogharimu kiasi cha Tshs.9,138,686,632.36 

Akiwasilisha mpango huo katika Baraza maalum la Madiwani la Kupitia mpango huo wa TARURA, Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Singida Eng. Christopher Njalika amesema fedha hizo zinatokana na fedha za Barabara (Road Fund) kiasi cha Tshs. 1,284,671,658.09 na fedha za Tozo 1,000,000,000 kwa Mwaka.

Alisema katika mpango huu TARURA inatarajia kutekeleza ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa kilometa 2.4, barabara za changarawe Km.107, ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua km.7 na ujenzi wa makalavati 95.

“Mpango huu unazingatia kwa kiasi kikubwa ukubwa wa barabara, wingi wa watumia barabara, uwepo wa taasisi, Pamoja na matatizo na kero za wananchi”, alisema.

Wakichangia mpango na bajeti hiyo, wajumbe wa bararaza hilo, walipongeza TARURA kwa kufanya mpango na bajeti yao kuwa shirikishi na kuridhika nayo. Aidha wameiomba TARURA pindi wanapopata fedha za nyongeza nje ya mpango huo kuzitumia katika Maeneo ambayo yameonekana kuwa na uhitaji mkubwa.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mhe. Yagi Kiaratu amezitaka taasisi za Serikali kama SUASA na nyinginezo katika Manispaa ya Singida kuiga mfano wa TARURA ili kuwezesha waheshimiwa madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchi kujadili na kutoa mapendekezo yao kwani wao ndio wanaozijua changamoto zinazowakabili wananchi kwa mapana zaidi.

“Ni vyema taasisi nyingine za Serikali zikaiga mfano wa TARURA  kwa kutushirikisha madiwani kwani  tutakuwa tumetatua changamoto kwa wananchi na kusukuma kwa Pamoja gurudumu la Maendeleo”, alisisitiza Mhe. Yagi

Aidha Mhe. Yagi alipongeza juhudi zinazofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kutatua changamoto mbalimbali za wananchi hasa uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati katika shule za msingi na sekondari nchini.

Amesema vyumba vya madarasa 42 vilivyojengwa kwa fedha za Maendeleo za UVIKO- 19 katika Manispaa ya Singida vimesaidia kupunguza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa na hivyo kuwataka wataalam katika Idara za elimu na Ofisi ya mchumi Manispaa kuhakikisha inawasilisha takwimu sahihi ili kutoa sura halisi ya upungufu uliopo.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.