• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TUME YA UCHAGUZI YASHAURI KATA YA MANDEWA KUGAWANYWA

Posted on: February 13th, 2023

Halmashauri ya Manispaa ya Singida imeshauriwa kuangalia uwezekano  wa kuigawa kata ya Mandewa ambayo imeelezwa kuongoza kwa  ukumbwa wa eneo na  idadi ya watu inayokadiriwa kuwa zaidi ya wakazi 40,000  hali inayoashiria kuwepo kwa ongezeko la idadi ya vituo vya kupigia kura katika Kata hiyo.

Ushauri huo umetolewa na timu kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikiongozwa na Leonard Tumua, ambaye ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu  na Utawala wa Tume hiyo ambao walifika kukagua vifaa kwa ajili ya zoezi la upigaji kura vilivyohifadhiwa katika stoo ya Halmashauri  sambamba na kutembelea kata za Mandewa na Misuna ambazo zinakadiriwa kuongoza kuwa ukubwa wa eneo, umbali  na wingi wa wakazi .

“Umbali, ukubwa na wingi wa watu katika kata ya mandewa na misuna kunaashiria ongezeko la vituo vya kupigia kura na uboreshaji wa daftari la mpiga kura” amesema Tumua.

Tumua pia ameshauri, zoezi la upangaji  vituo, liendane na taarifa za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ili kuepuka upotoshaji wa takwimu.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Jeshi Lupembe, amesema kuhusiana na suala la kugawa kata hizo mbili, tayari Manispaa imeliona na kwamba taratibu ama mchakato wa kuomba kuzigawa unaanzia kwenye kata husika.

Aidha Jeshi amesema tayari Halmashauri ya Manispaa imeanza mchakato wa kufuta vijiji katika Manispaa ya Singida zoezi linaloratibiwa na Mwanasheria wa Manispaa, Bahati Kikoti. Manispaa ya Singida ina jumla ya Kata 18,vijiji 19, mitaa 53 na vitongoji 83.

Naye Afisa Uchaguzi wa Manispaa ya Singida Edson Ndomba, ameshauri kuanza kwa mchakato wa kubaini vituo vipya vya kupiga kura mapema sambamba na vituo vya uboreshaji daftari la mpiga kura.

Aidha imeshauriwa pia suala la elimu kwa mpiga kura lipewe umuhimu kwa rika zote ili elimu iwafikie walengwa kwa kina hasa makundi ya vijana katika maeneo yote na hasa yale yenye idadi kubwa ya wakazi na pia kwa kuzingatia ukubwa na umbali uliopo.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Maulid Kiaratu, aliishukuru timu hiyo kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na kuwataka kubaini vituo vipya kwa wakati sambamba na kutoa elimu kwa wakazi wa Manispaa mapema ili wananchi waweze kujitokeza katika zoezi la kuboresha daftari la mpiga kura tayari kwa chaguzi zijazo.

Mstahiki meya alikiri kuwepo kwa Kata zenye maeneo makubwa, idadi kubwa ya wakazi na  umbali mrefu, na kusema ipo haja ya kuyagawa maeneo hayo.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.