• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAFANYABIASHARA WANNE WASHIKILIWA NA POLISI MANISPAA YA SINGIDA KWA KUFICHA NA KUPANDISHA BEI YA SUKARI

Posted on: January 24th, 2024

Kamati ya usalama wilaya ya Singida imefanya zoezi la kuwasaka wafanyabiashara waliopandisha bei ya sukari na kuificha kwa lengo la kuiuza kwa bei ya juu katika Halmashuri ya Manispaa ya Singida.Akiongoza zoezi hilo leo Januari 24, 2024,  Katibu Tawala Wilaya ya Singida Bi. Naima Chondo amesema, kulingana na mwongozo wa bei ya sukari uliotolewa hivi karibuni  na serikali, wafanyabiashara wa maduka ya jumla wanapaswa kuuza sukari kwa kilo kuanzia shilingi  2,650 hadi 2,800 wakati wale wanye maduka ya rejareja wanapaswa kuuza kuanzia shilingi 2,800 hadi 3,000 kwa kilo.Amesema awali kabla ya kufanyika kwa zoezi hilo, ilibainika kuwepo kwa wafanyabiashara wa rejareja wanaouza bidhaa hiyo  kwa shilingi 3,700 hadi 4,000 kwa kilo wakati wale wa maduka ya  jumla wameelezwa kupandisha bei hadi shilingi 185,000 kwa mfuko wa kilo 50.Bi. Chondo amesema kutokana na mabadiliko hayo ya bei serikali wilayani Singida imefanya msako wa wafanyabishara waliopandisha bei sambamba na kupekua stoo za baadhi ya wafanyabishara   na kufanikiwa kuwakamata wafanyabiashara wanne waliokiuka mwongozo wa bei zilizotolewa na serikali.“ Tunawaomba sana wafanyabiashara wa mkoa wa Singida  na hususani wilaya ya Singida kufuata taratibu, kanuni na sheria . Hii bidhaa pamoja na bidhaa nyingine zote zina bei elekezi, hivyo tuuze bidhaa hii kwa bei elekezi na waelewe pia kuficha bidhaa ni kosa la kuhujumu uchumi” amesisitiza Katibu Tawala.Naye wakala wa usambazaji wa sukari Mkoani Singida , Bw. Nagji amesema kulingana bei elekezi ya serikali, yeye anuza sukari hiyo  kwa shilingi 140,000 kwa Mfuko wa kilo 50 na kwamba tayari  gari mbili zilizobeba sukari zimewasili hivyo kushauri wafanyabiashara wengine kutoongeza bei.Mkuu wa Idara ya viwanda, biashara na uwekezaji Manispaa ya Singida, Erick Sinkwembe, amesema hakuna sababu kwa wafanyabiasha kuongeza bei kwani wakala wa usambazaji, amepokea mifuko 620 sawa na tani 32 za sukari leo Januari 24 na kwamba mifuko mingine 660 inatarajiwa kupokelewa Januari 25 katika Manispaa ya Singida na wilaya za jirani.Sinkwembe amewaasa wafanyabiashara kuzingatia bei elekezi ili kuondoa adha kwa watumiaji . “wakala anauza kwa bei elekezi na wafanyabiashara nao wanapaswa wauze kwa bei elekezi” amesema .Amewatoa hofu wananchi na wafanyabiashara kwa  kuwahakikishia uwepo wa sukari na kusisitiza kutopandisha bei wala kuficha bidhaa hiyo kwani sukari iliyopokelewa inatosheleza.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.