• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAFUGAJI WA KUKU SINGIDA WATAKIWA KUTUMIA CHANJO YA MIFUGO KUTOKA KATIKA VIWANDA VYA NDANI

Posted on: April 17th, 2023

Wafugaji Mkoani Singida wametakiwa kutumia chanjo inayotengenezwa na viwanda vya ndani, ili kukabili vita vya kiuchumi, kutokana na chanjo bandia ya kuku kuingizwa nchini, kwa lengo la kupunguza wingi wa mifugo hiyo.

Hayo yamebainishwa mkoani Singida na Dk, Charles Mayenga, Meneja wa kiwanda cha Chanjo ya Mifugo Tanzania (TVI-Kibaha), chini ya Wakala wa Maabara ya Veterinary Tanzania (TVLA), mwenye jukumu la kuzalisha na kusambaza Chanjo nchini.

Akiongea na wafugaji wa Kuku, wataalamu wa mifugo, wafanyabiashara na wamiliki wa maduka ya dawa za mifugo,katika Manispaa ya Singida, Dk.Mayenga amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapatia elimu washiriki juu ya uwepo wa chanjo bandia ya Matone (TEMEVAC 1-2), iliyoingizwa kwa ajili ya ugonjwa wa ’Mdondo’.

Amefafanua kuwa, chanjo ya TEMEVAC 1-2 ni muhimu katika kudhibiti ugonjwa wa ’Mdondo’ wa kuku, lakini chanjo bandia imeingizwa na hivyo kuathiri moja kwa moja uchumi wa mfugaji na Taifa kwa ujumla.

”Hii chanjo bandia ya TEMEVAC 1-2 inafanana sana na inayozalishwa na kiwanda cha Serikali cha TVI-Kibaha, na ukiichunguza sana ndipo utabaini tofauti iliyopo...ile ya bandia maandishi yake hayaonekani vizuri, ni meusi na yamechafuliwa sana,” amesema Dk. Mayenga.

Aidha Dk. Mayenga amefafanua kuwa, licha ya chanjo kutoka nje ya nchi kukabiliwa na changamoto nyingi, chanjo za ndani zina umuhimu zaidi kutokana na kuhimilimi mazingira husika, ambako zimetengenezwa.

Kutokana na hali hiyo Dk.Mayenga,ametoa rai kwa wadau hao kushirikiana pamoja katika kukabiliana na chanjo hiyo bandia, ili kulilinda soko la kuku wa asili wa mkoa wa Singida, kuku waliojizolea sifa na soko la uhakika nchini.

Baadhi ya washiriki,akiwemo mmiliki wa duka la dawa za mifugo,Dk. William Mafwere, ameipongeza serikali, kwa kuwapatia elimu juu ya kutambua chanjo bandia, jambo litakalolinda biashara kwa ajili yao na wateja wao.

Wakala wa Maabara ya Veterinary Tanzania (TVLA) hutengeneza aina saba za chanjo, ikiwemo ya Mdondo au Kideri (TEMEVAC), Homa ya mapafu ya Ng’ombe (CBPP), Homa ya mapafu ya mbuzi (CCPP), Kimeta (ANTHRAX), Kimeta na Chambavu (TECOBLAX), Chambavu (BLACKQUARER) na Kutupa Mimba (BRUCELLOSIS5-19.

Kwa mujibu wa Dk.Mayenga, chanjo hizo hupatikana makao makuu ya TVLA-Temeke Veterinari na ofisi za Kanda, ikiwemo Mwanza, Meatu, Tabora, Dodoma, Iringa, Sumbawanga, Kigoma, Tanga, Mtwara na Arusha.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.