• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAJASIRIAMALI SINGIDA WATAKIWA KUHAMISHIA BIASHARA KWENYE SOKO JIPYA LA UNYANKINDI

Posted on: September 20th, 2023


Manispaa ya Singida kwa kushirikiana wa wadau wake, wamewekeza miundo mbinu mbalimbali yenye thamani zaidi ya Sh.Milioni 900/=, katika soko la Unyankindi, ili kumaliza tatizo la uzalishaji wa taka, unaofanywa na wajasiriamali kwenye maeneo yasiyo rasmi na salama.

Kukamilika kwa miundombinu hiyo, itawalazimu wajasiriamali wa matunda na mbogamboga, waliopo soko la Msufini na wale wanaopanga bidhaa barabarani, sasa kuhamishia biashara zao kwenye soko jipya la Unyankindi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, mkuu wa mkoa wa Singida, Peter Serukamba, alitoa maelekezo kwa manispaa hiyo, kuhakikisha inasimamia usafi wa mji, sambamba na Baraza la Madiwani kutunga sheria ndogo, ili kudhibiti uchafu.

Akizungumzia hali ya soko ilivyo, Mwenyekiti wa ujenzi soko la Unyankindi, Ramadhan Isango, amefurahishwa kukamilika kwa miundombinu, ila ameomba Manispaa kushinikiza wajasiriamali wote kuhamia kwenye soko hilo, badala ya kuendelea kupanga bidhaa zao barabarani, hali inayohatarisha afya za walaji.

Ujenzi wa soko hili ulianza rasmi mwaka 2020 na kukamilika 2021, kwa agizo la serikali ya awamu ya sita, ilipoagiza wajasiriamali nchini watafutiwe maeneo rasmi…ni soko zuri lenye mahitaji yote, ikilinganishwa na kule wanakopanga bidhaa zao barabarani na kwenye makazi ya watu,”anasema Isango.

Mkuu wa idara ya viwanda, biashara na uwekezaji Manispaa ya Singida, Erick Sinkwembe, amesema jumla ya vibanda 300 na kituo cha magari kwa ajili ya kushushia mizigo, tayari ujenzi wake umekamilika katika soko la Unyankindi, hivyo ameawataka wajasiriamli kuhamia sokoni hapo kupunguza msongamano na taka, eneo la katikati ya mji.

Sinkwembe amesema kuendelea kupanga bidhaa zao eneo la Msufini, pembezoni mwa barabara na katika nyumba za watu, inahatarisha Maisha yao, hivyo akatoa rai waende kwenye maeneo rasmi yaliyotengwa, ikiwemo soko la Unyankindi, Mahembe, usafirishaji Majengo, stendi ya vumbi Misuna na Ukombozi.

“Wafanyabishara watakapohamia kwenye maeneo hayo, itahamasisha soko kukua, maa yake soko ni watu, hata wateja wanapoenda pale, sehemu hiyo itakua na hata taasisi zinazotoa mikopo ni rahisi kukopesha, kutokana na mjasiriamali kuwa na kituo rasmi cha kazi yake,” alisema Sinkwembe.

Kaimu Mkuu wa kitengo cha usafi na udhibiti wa taka, Manispaa ya Singida, Shuku Kaishwa, amesema uzalishaji taka hivi sasa ni tani 120 kwa siku, huku kiwango cha uzoaji kikiwa ni asilimia 60 hadi 75 kwa siku, hivyo iwapo wajasiriamali hao watatekeleza agizo la kwenda kwenye maeneo rasmi, itasaidia kuuweka mji katika hali ya usafi.

Kaishwa amesema, kwa mujibu wa sheria ya afya na usafi ya manispaa 2019, ipo wazi, ikimtaka kila mfanyabiashara kulipia ushuru wa ada ya taka, lakini kwa wajasiriamali hao kutokuwa kwenye maeneo rasmi, wanakuwa ni sehemu kuu ya uchafuzi wa mazingira, kutokana na kuwemo sehemu ambazo siyo rasmi.

“Wafanyabiashara hawa, wao wakati mwingine kutokana na kutokuwa maeneo rasmi, utakuta wanafanya shughuli zao kwa muda ambao saa za kazi kwa watumishi wa serikali umeisha, hivyo hata kudai ushuru wa ada ya taka, inakuwa vigumu kukusanya, lakini wakiwa maeneo rasmi, ni rahisi kufuatilia na kupata ada hiyo,”anasisitiza Kaishwa.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara mijini na vijijini, wilaya ya Singida, mhandisi, Lambert Bayona, amesema sheria ya barabara ya mwaka 2007, inazuia na inadhibiti mtu au kikundi chochote bila ya kuwa na kibali cha mamlaka husika kufanya chochote, hivyo wafanyabiashara hao kuweka bidhaa zao barabarani, ni kosa kisheria na wanapaswa kuondolewa, ili kutii matakwa ya sheria.

Amesema wafanyabiashara wa eneo la Msufini, wanatakiwa kuiacha wazi barabara, kwa ajili ya matumizi husika ikiwemo wananchi kwenda kupata huduma muhimu katika sehemu hiyo, yenye huduma nyingi za kijamii, ikiwemo zahanati, ofisi za chama (CCM), shughuli za ibada na masuala mengineyo ya kijamii.

 Kutokana na hali hiyo, mhandisi Bayona, ameiomba manispaa ya Singida, kusimamia zoezi hilo, kwa kuwaondoa wote wanaoendesha biashara kwenye barabara, ili wapishe na waende walikotengewa na serikali, kwa ajili ya shughuli zinazoendana na shughuli zao.     

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.