• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAKULIMA NA WAFANYABIASHARA SINGIDA, WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA KWA TIJA

Posted on: September 8th, 2024



Serikali ya Mkoa wa Singida imewataka wakulima na wafanyabiashara kuendelea kutumia mfumo wa stakabadhi za ghala kwa tija kubwa ili kuwaepusha na walanguzi wa mazao ya biashara na kuimarisha biashara yao.


Akizungumza (6 Septemba, 2024), Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Halima Dendego, amesema kuwa mfumo huu umeanza kutekelezwa rasmi katika msimu wa 2024/2025 mkoani humo.


Aidha ameeleza kuwa utekelezaji wa mfumo huo unafuatia maagizo yaliyotolewa na serikali kupitia mwongozo wa biashara ya mazao kama dengu, mbaazi, na ufuta, ambao umetolewa chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), Tume ya Ushirika, Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala na Soko la Bidhaa kupitia toleo la tatu la mwaka 2024.


Mkuu wa Mkoa pia alibainisha kuwa mwongozo huu mpya unalenga kudhibiti biashara ya mazao na kuwahakikishia wakulima na wafanyabiashara masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi. Kupitia mfumo huu, wakulima watapata bei nzuri kwa mazao yao ikilinganishwa na miaka iliyopita, na hivyo kuongeza mapato yao.


Amefafanua kuwa, bei ya zao la dengu ambayo ilikuwa inauzwa kati ya TZS 900 hadi 1300 kwa kilo katika msimu wa 2023/2024, sasa inauzwa kati ya TZS 1,670 hadi 2,060 kwa kilo katika msimu wa 2024/2025 kupitia mfumo wa stakabadhi za ghala.


Faida nyingine za mfumo huu ni pamoja na ongezeko la mapato kwa halmashauri, udhibiti wa utoroshaji wa mazao, na kutoa uhakika wa takwimu kwa serikali. Mfumo huu pia umewezesha upatikanaji rahisi wa mikopo kwa wakulima na kuongeza masoko ya uhakika ya ndani na nje ya nchi.


Hata hivyo, amesema, ubora wa mazao umeimarika kwa kiasi kikubwa kutokana na mfumo huu ambao unazingatia taratibu na viwango bora vya usafirishaji na uhifadhi wa mazao, pia mfumo wa stakabadhi za ghala umeleta mapinduzi makubwa katika biashara ya mazao mkoani Singida.


Serikali ya Mkoa wa Singida inaendelea kushirikiana na wadau wote muhimu ili kuhakikisha mfumo huu unatekelezwa kikamilifu na kuleta matokeo chanya kwa wakulima na wafanyabiashara. Hii ni hatua muhimu.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • INEC YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI

    May 14, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA VYA SIASA WALA KIAPO CHA UTII

    May 12, 2025
  • MANISPAA YA SINGIDA YATAKIWA KUPIMA MAENEO KABLA YA KUTEKELEZA MIRADI

    May 09, 2025
  • “PONGEZI KWAKO, RC HALIMA DENDEGO”

    May 09, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.