• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WALENGWA WASIMULIA NAMNA TASAF ILIVYOBADILISHA MAISHA WAISHUKURU SERIKALI

Posted on: August 17th, 2024



Walengwa wa Mradi wa TASAF wameeleza jinsi mradi wa vitofali (pavement) ulivyobadilisha maisha yao na kutoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa ushirikiano na msaada wao.


Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi wa vitofali uliohitimishwa katika Shule ya Msingi Imbele, Manispaa ya Singida, walengwa walisisitiza umuhimu wa mradi huo. Mradi huo, uliofadhiliwa na TASAF, umeendeshwa na walengwa 44, ambapo mwanaume alikuwa mmoja pekee. Walengwa walihusika katika ufyatuaji wa vitofali na kutengeneza eneo la utawala la shule hiyo ili kupunguza vumbi na tope wakati wa masika.


Mradi huu umekuwa na mchango mkubwa kwa walengwa, ambao wamepata elimu ya ufundi ya ufyatuaji vitofali na wanaamini ujuzi huu utaendelea kuwa na manufaa kwao. Caroline Francis, mmoja wa walengwa, anasema: “Mradi wa TASAF umenisaidia kubadili maisha yangu. Hadi sasa nimeweza kujenga nyumba na pia nafanya biashara ndogondogo. Nashukuru Serikali yetu kwa kuendelea kutuunga mkono.”


Mwinyi Masumbuko, mwanaume pekee kati ya walengwa 44, ameongeza: “Nimepita katika miradi mingi ya TASAF, lakini huu umeweza kumsaidia mtoto wangu kumaliza kidato cha nne na pia nimemudu kupata kiwanja. Ingawa fedha ni chache, tunapambana na tunashukuru Serikali.”


Mratibu wa TASAF wa Manispaa ya Singida, Stara Beka, amesema: “Huu ni mradi mpya wa TASAF na umeleta mabadiliko makubwa. Walengwa wamepata ujuzi utakaowasaidia sana. Wengi tayari wapo tayari kuanzisha vikundi vitakavyokuwa msaada kwao. Tunashukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa ruzuku kwa walengwa hawa.”


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Imbele, Edina Daudi, amesema: “Kama familia ya Imbele, tumenufaika sana na mradi huu. Tulikuwa tunakumbana na tatizo la vumbi na mmomonyoko wa udongo, lakini mradi huu umeleta mabadiliko makubwa. Tunamshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan na timu nzima ya TASAF kwa kubadili maisha ya walengwa.”

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.