• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WALIMU WAKUU MANISPAA YA SINGIDA WATAKIWA KUDHIBITI UDANGANYIFU WA MITIHANI

Posted on: July 7th, 2022

HALMASHAURI ya Manispaa ya Singida imewataka walimu Wakuu na walimu wa taaluma wa shule za msingi, kujipanga vyema katika maandalizi ya mtihani wa kujipima wa taifa, ikiwa ni maandalizi ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu, hapa nchini.

Afisa Elimu Msingi Omari Maje, alisema hayo jana 6 julai, 2022, wakati akifungua kikao kazi cha tathmini, mitihani ya utimilifu  ngazi ya mkoa, kilicho husisha walimu Wakuu, walimu wa taaluma na maafisa elimu kata, kilichofanyika ukumbi wa shule ya msingi Tumaini maalumu kwa wanafunzi wasiosikia.

Maje aliwataka washiriki hao kujifunza kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kupitia matokeo hayo, hivyo kuepuka kujirudia kwa kosa kwenye mtihani ujao wa taifa, huku akisistiza kwamba matokeo mazuri yanawezekana iwapo wataepuka udanganyifu.

“Mimi sio muumini kabisa wa udanganyifu, na ninyi mnapaswa kuwa hivyo, waumini wa ukweli…ukiwa mkweli utafanikiwa katika kazi, na mikakati yetu itawezekana kwa kuhakikisha kwa Pamoja tunainua kiwango cha elimu kwa manispaa yetu” alisema Maje

Aidha, Afisa elimu huyo alitumia fursa hiyo kuwataka washiriki hao kutumika vizuri fursa hiyo na kuzibaini changamoto zinazowakabili walimu zinazosababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu, katika masomo wanayofundisha.

Afisa elimu huyo pia alimpongeza mwalimu mkuu wa shule ya msingi kibaoni, mwalimu wa taaluma na Afisa elimu kata ya Kindai, kwa kazi nzuri waliyofanya, hadi shule hiyo kutoa mwanafunzi wa kwanza kimkoa katika mtihani wa utimilifu wa mkoa, hivyo kuiletea heshima kubwa Manispaa ya Singida.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Ndg. kulanga Kanyanga, aliwapongeza washiriki kwa mafanikio waliyopata, na kueleza kuwa Ofisi yake inaendelea na mchakato wa sera ya motisha, kwa shule na walimu watakaofanya vizuri. Aidha alibainisha kuwa hata kwa walimu ambao shule zao zitafanya vibaya nao watapata motisha hasi ili iwe funzo na baadaye waongeze juhudi katika kuinua kiwango cha elimu ili kukwepa motisha hiyo.

“ Ninyi mmeaminiwa kwa ajili ya kuhudumia watoto, timizeni wajibu wenu kama ambavyo serikali inatimiza wajibu wake kwenu…” alisema Kulanga.

Akizungumzia suala la malipo ya mapunjo ya mishahara kwa watumishi, Kulanga alisema kuwa, hadi sasa jumla ya watumishi 136 tayari wameshalipwa mapunjo yao yanayofikia kiasi cha Tshs. 187,420,941/51, yakiwa ni malimbikizo kwa mishahara ya miaka ya nyuma, hadi sasa.

Hata hivyo, Kulanga aliwataka watumishi wote kuwajibika  ipasavyo katika majukumu yao, kwani serikali wanayoitumikia ni sikivu na inawajali, na kwamba mbali na mapunjo yao, hata madai mengine pia yanashughulikiwa kulingana na taratibu, kanuni na sheria za serikali.

“ Ninyi wenyewe ni mashuhududa  baadhi ya walimu hapa walikuwa wanadai malimbikizo ya miaka mpaka 10  iliyopita na  tayari wamelipwa haki zao…” alisema Kulanga.

Naye Mthibiti Ubora wa Elimu Manispaa ya Singida Ndg. Seif Mziray, alitumia fursa hiyo kuwaasa washiriki hao, kutotumia kigezo cha upungufu wa walimu kama sababu ya shule zao kufanya vibaya kwenye mitihani, na akasisitiza watimize vema wajibu wao.

“ Msijifiche kwenye mwamvuli wa upungufu wa walimu, Mwalimu kama ana vipidi 30, ni wajibu wake kuhakikisha anafundisha vipindi vyote, lakini sababu ya upungufu wa walimu, kwa kweli hiyo sio sababu ya msingi” alisema Mziray

Aliwataka walimu kuhakikisha wanafuatilia mahudhurio ya wanafunzi ili yapande, na kwa shule ambazo mahudhurio ni dhaifu, basi  ni jukumu la uongozi wa shule kushirikisha kamati za shule, wazazi, Serikali za Vijiji, mtaa na kata, kumaliza tatizo hilo.

Manispaa ya Singida ilipata asimia 67.69 ya ufaulu katika mitihani ya utimilifu kimkoa, ambapo jumla ya wanafunzi 5,339 walifanya mitihani hiyo kati ya 5,529 waliosajiliwa Baraza la mitihani  mwaka 2016.

Katika mafunzo hayo, jumla ya walimu wakuu 44, walimu wa taaluma 43 na maafisa elimu Kata 9 walishiriki kikao hicho cha tathmini, kwa lengo la kuboresha sekta ya elimu ya msingi, Manispaa ya Singida.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.