• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANAFUNZI NA WANANCHI WA MTAA WA KIBAONI KUONDOKANA NA ADHA YA AJALI ZA MARA KWA MARA

Posted on: April 27th, 2023

ZAIDI ya wanafunzi 2,000 wa shule ya Msingi Kibaoni, Mahembe na maelfu ya wananchi wa kata ya Kindai, wataondokana na ajali za barabarani za mara kwa mara, baada ya serikali kujenga kivuko cha chini (Underpass), kwenye eneo la Kibaoni, katika Manispaa ya Singida.

Kaimu Meneja wa Tanroads mkoa wa Singida, mhandisi Yohannes Mbegalo, alisema ujenzi wa kivuko hicho chenye urefu wa mita 24.5, upana mita 4.6 na kimo mita 2.4, utakamilika juni 22 mwaka huu, na utagharimu Sh. Milioni 427.8/=, na hivyo kuokoa maisha ya mtu mmoja anayepoteza maisha, kila baada ya miezi mitatu.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, pamoja na wananchi, kufuatia ziara ya Mkuu huyo wa mkoa alipokwenda kuona maendeleo ya ujenzi, Mbegalo alisema kuwa, Wakala wa Barabara (TANROADs), aliamua kuchukua hatua ya kujenga kivuko cha chini cha waenda kwa miguu eneo la barabara kuu ya Dodoma – Singida  ili kuwezesha waenda kwa miguu kuvuka kwa usalama.

“Hapa licha ya kuwa na shule hizi, kuna wananchi wengi na Makanisa, ambayo waumini huvuka kuwahi ibada na hatimaye hukutwa na kadhia ya kugongwa na magari, katika barabara hii ya Dodoma-Singida, eneo la Kibaoni.…,”alifafanua Mbegalo.

Baadhi ya Wazazi, akiwemo Rachel Chaka, Theophil Macarius na Diwani wa Kata ya Misuna, Hamisi Kisuke, walisema kukamilika kwa kivuko, ni nafuu kwa wanafunzi wanaopoteza maisha, kutokana na uzembe wa madereva kwa kushindwa kuzingatia alama za usalama barabarani.

Hata hivyo, wazazi hao wameiomba Serikali, kujenga kivuko kingine cha juu, karibu na eneo la Kibaoni, ambacho kitasaidia wananchi kuvuka nyakati za usiku, ili kuepuka vibaka watakaolazimika kuvizia watu watakaopita katika daraja la chini (Underpass).

“Tumeelezwa kivuko hiki kitawekewa taa na kamera ili kudhibiti wezi, lakini sisi tunaomba tujengewe pia daraja la juu ili tuwe tunapita wakati wa usiku, kwasababu hili hapa la chini sisi usiku itakuwa ni hatari, tutakabwa na vibaka,” alisema Kiranga.

Akizungumza na wanafunzi na wananchi baada ya kukagua ujenzi wa kivuko hicho, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, aliwataka kutumia kivuko hicho, ili kuepuka ajali.

Mkuu huyo wa Mkoa alimtaka Wakala wa Barabara nchini , kuhakikisha amamsimamia vyema Mkandarasi aliyepewa jukumu la ujenzi wa mradi, aweze kukamilisha mapema zaidi, ili wananchi wanufaike na kivuko hicho.  

Ziara hii ya Mkuu wa mkoa katika mradi wa kivuko cha chini cha waenda kwa miguu, ni mwendelezo wa shughuli mbalimbali zilizopangwa kutekelezwa katika wiki ya maadhimisho kuelekea kilele cha sherehe za miaka 59 ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.

Shughuli zilizotangulia kutekelezwa tangu mwanzo wa wiki, katika Manispaa ya Singida  ni pamoja na usafi wa mazingida, uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa zahanati ya Isomia, uzinduzi wa wiki ya chanjo, mtahalo wa masuala ya Muungano uliohusisha wanafunzi wa shule 5 za sekondari katika manispaa ya Singida pamoja na uchangiaji damu salama

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.