• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI MANISPAA YA SINGIDA WAPONGEZA JITIHADA ZA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KATIKA KUSOGEZA HUDUMA KARIBU NA WANANCHI

Posted on: June 23rd, 2022

HALMASHAURI ya Manispaa ya Singida imepokea zaidi ya Sh. Bilioni 3.3 katika kipindi cha mwaka huu wa fedha (2021/22), kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mstahiki Meya, Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu amesema hayo, wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Binilith Mahenge katika Manispaa hiyo ambapo aliongea na wananchi kupitia  mkutano wa hadhara  uliofanyika viwanja vya stendi ya zamani, katika Manispaa ya Singida.

Mheshimiwa Kiaratu alisema kuwa kati ya fedha hizo, zaidi ya Sh. Bilioni 1.6 zilitekeleza miradi mbalimbali kwa sekta ya elimu, ikiwemo ujenzi wa sekondari mpya ya kata ya  Uhamaka. Kata ya Uhamaka ni kata pekee kati ya kata 18 za Manispaa ya Singida ambayo haikuwa na shule ya sekondari  hivyo kulazimu wanafunzi katika kata hiyo kupelekwa katika shule za kata jirani hivyo kutembea umbali mrefu.

Aidha amesema kwa kipindi hicho Manispaa ya Singida imejenga vyumba 62 vya madarasa, kati ya hayo  42 ni ya shule ya sekondari na mengine 16 ya shule za msingi, pia fedha hizo zimetumika kujenga vyumba vya maabara na kukamilisha vyumba vya maabara vilivyokwishajengwa na kufikia hatua mbalimbali za ukamilishaji.

Mstahiki Meya alifafanua kuwa katika sekta ya afya, zaidi ya Sh. Bilioni 1.4, zimetekeleza miradi ya afya, ukiwemo ujenzi wa vituo vipya vya afya katika Kata za Mandewa na Unyambwa  ambavyo kila kituo kinagharimu kiasi cha Sh. Milioni 500. Aidha  alisema kuwa, Sh. Milioni 300 zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya ya upasuaji na wodi ya mama na mtoto katika vituo vya Afya  vya Sokoine  kata ya Misuna na Mtisi Kata ya Mtamaa ambapo ujenzi wake bado unaendelea, lengo likiwa ni kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, tunaishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan…ametupatia pia shilingi bilioni 1,400,000,000/- za ujenzi wa zahanati 2 za Unyinga na Kisasida , ujenzi wa majengo ya upasuaji na wodi ya mama na mtoto katika vituo vya afya vya Sokoine na Mtisi, ujenzi wa vituo vya afya  Kata za Unywambwa na  Mandewa” alibainisha Meya.

Kuhusu ujenzi wa miundombinu ya barabara, mstahiki meya alisema kuwa, TARURA imepokea zaidi ya shilingi milioni 268, kwa ajili ya kuzifanyia matengenezo barabara za manispaa, ili ziweze kupitika wakati wote wa mwaka.

Akifafanua kuhusu ukusanyaji wa  mapato ya ndani ya Manispaa Mhe. Yagi  amesema kuwa, mpaka sasa Manispaa ya Singida imefanikiwa kukusanya mapato ya ndani asilimia 95.7, ambayo ni mapato huru, ambayo pamoja na shughuli zingingine za maendeleo pia yameiwezesha Halmashauri  ya Manispaa kufanikisha zoezi la anwani za makazi zoezi lililogharimu zaidi ya Sh. Milioni 270 za mapato ya ndani.

Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binirith Mahenge, Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi  Paskasi Muragili, alibainisha kuwa, miradi yote inayotekelezwa na serikali, inagusa moja kwa moja kero za wananchi, hali inayoonyesha serikali inawajali wananchi  wake.

“Mkuu wa mkoa, miradi hii ni muhimu sana katika kumkomboa Mtanzania…hapa unaona kituo cha afya Sokoine, kinahudumia wajawazito 600 mpaka 700 kwa mwezi wanaokwenda kujifungua, kwa kweli kinabeba mzigo mkubwa sana wa kuhudumia akina mama,”alisema.

Mhandisi Muragili alifafanua kuwa, serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara, kutawanya umeme, maji na huduma nyinginezo za umma, ili kumrahisishia mwana-Singida kupata huduma bora zaidi na hivyo kustawisha maisha ya wananchi kwa ujumla.

Pia Mhandisi Muragili alimtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida kupita na kuhakiki maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya  wafanyabiashara wadogo,  ili kuona hali ya mazingira, lengo likiwa ni kubaini changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi  kabla ya kuwarejesha katika maeneo hayo.

Akizungumza na wananchi, mgeni rasmi katika mkutano huo wa hadhara, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binirith Mahenge,  aliwataka wananchi kujitokeza kueleza kero zao kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia katika kuboresha huduma kwa jamii  ikiwa ni pamoja na maendeleo katika nyanya zote.

“Sasa nimekuja na wenzagu hawa wote, ni zamu yenu mtuambie jamani bidhaa zetu zikoje, tunakosea wapi sisi , mseme, nimekuja mimi mwenyewe mkuu wa mkoa,sawa ndugu zangu, mtuchambue vizuri kama bidhaa haitoshi, semeni hapo haitoshi , kuna changamoto, semeni ili tuboreshe,”alisema Dk. Mhenge.

Katika kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kutosha kuhusu shughuli za serikalii, Mkuu wa Mkoa alitoa fursa kwa Wakuu wa Taasisi mbalimbali kuelezea mipango ya utekelezaji wa shughuli za kuletea wananchi maendeleo ya taasisi zao ambayo kwa namna moja ama nyingine ilijibu kero nyingi zilizowasilishwa na wananchi

Dk. Mahenge pamoja na kupokea kero za wananchi  aliweza kutoa majibu ya kero hizo sambamba na kutoa maelekezo ambapo aliagiza wataalamu wa ugani kuhakikisha wanazitumia vema pikipiki walizopewa na serikali kwa kuwafikia wakulima ili kujua mahitahi yao pia ushauri wa kitaalamu  ili kuleta tija katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Pamoja nao aliwaagiza pia wataalamu wa idara ya ardhi, kufika eneo la uwanja wa ndege ili kuitambua mipaka ya uwanja huo kwa lengo la  kuepusha uwanja huo kuendelea kuvamiwa na wananchi wanaoendeleza makazi na kuongeza kuwa  zoezi hilo  ni sehemu ya maandalizi ya utanuzi wa uwanja huo na kuwataka wataalamu hao kumpatia mrejesho ndani ya siku saba.

Katika hatua nyingine, Dk. Mahenge alitambua umuhimu wa wasanii katika kuhimiza shughuli za maendeleo katika sekta zote hivyo kuagiza kufanyika kwa kikao cha wasanii wote wa mkoa wa Singida na idara ya Utamaduni mkoa, ili kupitia changamoto, kutatua na kujadili namna bora za kufikia jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo kwa njia ya sanaa.

Mkuu wa Mkoa alihitimisha mkutano wake, kwa kuwataka wananchi kuunga juhudi za serikali kupitia  miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa, na kuwataka  kumuunga  mkono Mstahiki Meya wa Manispaa, kwa juhudi anazofanya katika kuiletea maendeleo Manispaa ya Singida.

 

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MEI MOSI - MAJALIWA

    April 30, 2025
  • KIKWETE AFUNGA MICHEZO UWANJA WA CCM LITI

    April 30, 2025
  • "UMUHIMU WA MFUMO BORA WA USALAMA WA AFYA KAZINI"

    April 28, 2025
  • "UMUHIMU WA MFUMO BORA WA USALAMA WA AFYA KAZINI"

    April 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.