• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Mipangomiji
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu
      • Idara ya Maji na Usafi wa Mazingira
      • Idara ya Utumishi na Utawala
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WATUMISHI MANISPAA YA SINGIDA WAASWA KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOWEA

Posted on: June 14th, 2022

Watumishi Manispaa ya Singida wametakiwa kuacha kufanya kazi kwa mazowea na kuwajibika ipasavyo kwa wananchi ambao wapewa dhamana ya kuwahudumia kupitia utaalamu wao.

Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mhe. Yagi Kiaratu (13.06.2022) wakati akizungumza na watumishi wa kata tatu za Ipembe, Majengo na Misuna katika kikao kazi kilichoandaliwa na ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ikiwa ni utaratibu uliowekwa wa kuzungumza na watumishi katika kata.

Mhe. Yagi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Majengo alisema vikao kama hivi ni Sehemu ya kukumbushana wajibu wa kiutumishi ambao kwa namna moja ama nyingine watumishi wamekuwa wakijisahau ama kurithi masuala ya kiutendaji ambayo ni kinyume na taratibu za kiutumishi kutoka kwa watangulizi wao hivyo kuathiri utoaji huduma kwa Jamii.

“Forum kama hii inawakumbusha kuwajibika kwa kada mnayoitumikia pia kwa Jamii inayowazunguka ili iendelee kujenga imani na nyie kwa uadilifu unaouonesha” alisisitiza Mhe. Yagi

Alisema elimu nzuri na utaalamu walionao Watumishi hauna faida kama hawataweza kuionesha kupitia huduma bora kwa Jamii na mahusiano mazuri baina yao na Jamii inayowazunguka na kuongeza kuwa ni jukumu la watumishi kujenga taswira nzuri ya Serikali kupitia uwajibikaji wao.

“Tumieni nafasi hii kuzungumzia changamoto zinazowakabili ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaathiri utendaji kazi wenu” alisisitiza.

Aidha amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa pamoja na masuala mengine kuhakikisha usalama wa watumishi unakuwepo wawapo kazini hii ikiwa ni pamoja na mazingira wanayofanyia kazi na kutatua changamoto zinazowakabili kwa wakati.

Mhe. Yagi amesema ofisi ya Mkurugenzi ina wajibu wa kujenga mahusiano mazuri na vyama vya wafanyakazi ili kuweza kushirikiana pamoja katika kutatua migogoro ya wafanyakazi na changamoto zinazowakabili kabla ya kupelekana mbele ya sheria.

Ametoa rai kwa Watumishi kuwajibika ili kuleta matokeo chanya na kuongeza kuwa ni aibu kwa mtumishi kulalamikia Serikali wakati hana alichoitendea Serikali ambacho kinapimika na kusema kuwa haki ni lazima iendane na wajibu.

“kabla hujailalamikia Serikali hebu jiulize wewe umeitendea nini Serikali”, alisistiza mhe. Yagi

Alisema watumishi wa Serikali popote walipo ni jeshi la Mhe. Rais na wanawajibika kuitendea haki Serikali kwa kutoa huduma iliyo bora kwa wananchi na kuitendea haki nafasi yake aliyopewa kama mtumishi wa umma.

“Watumishi mnauza huduma hivyo wateja wenu ambao ni Jamii lazima waridhike na huduma mnazotoa kupitia lugha nzuri, uwajibikaji bora na mahusiano mazuri” aliasa Mhe. Yagi

Mkakati wa Manispaa ya Singida wa kuzungumza na watumishi wa kata ni endelevu  ili kuiwezezesha Halmashauri kubaini changamoto zinazowakabili watumishi wake na hivyo kuzitatua kwa wakati na kuboresha utendaji kazi wa watumishi.

Matangazo

  • TANGAZO LA UPANGAJI UPIMAJI NA URASIMISHAJI WA MAENEO KWA NJIA SHIRIKISHI June 16, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI March 07, 2022
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA MANISPAA YA SINGIDA KWA SHULE 2021 November 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA MANISPAA YA SINGIDA KWA KATA 2021 November 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • WANANCHI MANISPAA YA SINGIDA WAPONGEZA JITIHADA ZA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KATIKA KUSOGEZA HUDUMA KARIBU NA WANANCHI

    June 23, 2022
  • RC SINGIDA: SIMAMIENI VIZURI VYANZO VYA MAPATO ILI KUPUNGUZA HOJA ZA UKAGUZI

    June 15, 2022
  • WATUMISHI MANISPAA YA SINGIDA WAASWA KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA

    June 14, 2022
  • WATUMISHI MANISPAA YA SINGIDA WAASWA KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOWEA

    June 14, 2022
  • Tazama Zote

Video

Waziri Jafo atoa maagizo mazito kwa ma-RAS, ma-DED, Wakuu wa idara na maasifa mawasiliano serikalini
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.