• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WATUMISHI SEKTA YA AFYA WATAKIWA KUWAJIBIKA, WABINIFU KUMALIZA CHANGAMOTO

Posted on: August 12th, 2023

Mkurugenzi wa afya, ustawi wa jamii na lishe ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Ntuli Kapologwe, amewaka viongozi na watumishi wa umma nchini, hasa sekta ya afya, kuwajibika na kuwa wabunifu ili kupunguza changamoto za utoaji huduma za afya.

Dkt Ntuli, amesema hayo leo Agosti 12, 2023, katika kikao cha majumuisho kilichohusisha halmashauri zote saba za mkoa wa Singida, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa, kila mtu kwa nafasi yake anapaswa kuwajibika kwenye eneo lake la kazi, ili kubaini mapungufu na kuboresha kwa kuweka mazingira bora na wezeshi ya  upatikanaji kwa huduma ya afya kwa jamii,

“Tusipowajibika ipasavyo katika kutoa huduma, ni sawa na kumchonganisha Mheshimiwa Rais na wananchi wake…sitamvumilia mtu anayeshindwa kuwajibika kwa ajili ya maendeleo ya Taifa,”amesema Dkt. Ntuli.

Amesema kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya kazi kubwa katika kuwajali wananchi wake, kwa kuwajengea vituo vya afya, zahanati na hospitali, lakini amehakikisha kuna uwepo wa kutosha wa dawa, vifaa tiba na watumishi.

Kutokana na hali hiyo, Dkt. Ntuli amewataka wataalamu wa afya kuhakikisha, wanawahudumia wananchi ipasavyo, ili kuondoa mapungufu ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na wananchi.

Kuhusu watumishi wapya wanaoajiriwa katika sekta ya afya, Dkt. Ntuli ametoa agizo la kuhakikisha wanapelekwa kwenye vituo walikopangiwa, badala ya kuachwa makao makuu, hali inayowakosesha wananchi haki ya kupata huduma muhimu za kitabibu, pia ni njia moja wapo ya kuwajengea uzoefu watumishi hao katika suala zima la utoaji huduma.

Aidha Dkt. Ntuli ameasa watumishi kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano, kwa ngazi zote, lengo likiwa ni kufanikisha kile kilichokusudiwa na serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi, kinapatikana.

Pia Dkt. Ntuli amewataka watumishi kuelezea huduma mbalimbali zinazotolewa na vituo vinavyotoa huduma za afya, ili kushawishi wananchi, kuzifuata na hivyo kuondokana na dhana kwamba vituo vya afya vya umma, havitoi huduma bora.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Jeshi Godfrey Lupembe, amemhakikisha Mkurugenzi wa afya, ustawi wa jamii na lishe ofisi ya OR – TAMISEMI kuwa atsimamia suala zima la uwajibikaji ili kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa kiwango kilichokusudiwa

“ nimepokea maelekezo, na ninaahidi kuyafanyia kazi……. Hata sisi wote hapa tumeanzia chini lakini kutokana na uwajibikaji mzuri leo tupo hapa tulipo…” amesema Jeshi.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.