• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WIKI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU YAENDELEA KWA SHUGHULI ZA USAFI KATIKA MANISPAA YA SINGIDAGIDA

Posted on: December 6th, 2022

Wakazi wa Manispaa ya Singida leo tarehe 6 Desemba 2022 wameendelea na wiki ya  maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika kwa  kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Singida

Akiongoza zoezi la Usafi, Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Mulagiri,  akiwa pamoja na watumishi  na wananchi wa Manispaa ya Singida, amewataka wananchi kujenga tabia ya kufanya usafi wao wenyewe bila kusuribiri matukio muhimu.

Mulagiri amesema maagizo aliyotoa yanalengo moja la kuuweka mji katika hali ya usafi  kama ambavyo wananchi wake walivyo na utamaduni wa usafi hali itakayoiweka Singida kuwa  miongoni mwa mikoa/ wilaya zinazoongoza kwa usafi hapa nchini.

Amesema eneo lolote la biashara ama makazi litakalokutwa chafu mhusika wa eneo atatozwa faini  kuanzia Sh. 50,000 hadi 300,000 hivyo kuwataka wananchi wote kuzingatia hilo ili kuepuka faini hizo.

“faini itatozwa kwa yeyote atakayekutwa ameacha eneo lake chafu Iwe ni sehemu ya biashara ama makazi kuanzia sh. 50,000 hadi 300,000 kutegemeana na wingi wa uchafu uliachwa mbele ya eneo lako” amesisitiza Mkuu wa Wilaya

Aidha Mhandisi Mulagiri ametoa rai kwa wananchi kuwakamata wale wote watakaokutwa wakichafua mazingira kwa kutupa taka ovyo ama kujisadia  maeneo ambayo yasiyo rasmi kuwakamata na kuwatoza faini isiyopungua Sh. 50,000 na kusema kuwa yeyote atakayemkamata mchafuzi wa mazingira kupewa motisha ya Sh. 10,000 papo hapo

Pamoja na hayo, Mkuu huyo wa wilaya ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuagiza  fedha Zaidi ya Sh. Milioni 900 zilizokuwa zitumike katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru tarehe 9 Desemba kutumika katika mradi wa ujenzi wa mabweni katika shule 8 za wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Naye Naibu Meya wa Manispaa ya Singida Hassan Mkata, amemtaka Mkurugenzi kuhakikisha anasimamia vyema maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa wilaya Mhandisi Mulagiri huku akiwataka wananchi na hasa wafanyabiashara kuhakikisha wanatekeleza maagizo yaliyotolewa.

“……isije ikafika mahali mkatozwa faini mkaanza kulalamika mnaonewa na serikali, nawaomba sana tuzingatie taratibu, sheria na kanuni tulizojiwekea wenyewe za mwaka 2019 kuhusu usafi wa mazingira” amesema Mkata

Aidha Naibu Meya ameupongeza uongozi wa soko kwa uhamasishaji wa zoezi la usafi hali iliyofanya watu kujitokeza kufanya usafi eneo la soko kuu Kata ya Ipembe

Zoezi hili la usafi ni  moja ya njia ya kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassani katika kudumisha Amani na umoja kwa maendeleo ya nchi yetu kama ambavyo kauli mbiu ya ya Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika inavyohimiza “ Amani na Umoja, nguzo ya Maendeleo yetu”

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.