• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WILAYA YA SINGIDA YAJIZATITI UFUNDISHAJI KWA NJIA YA TEHAMA

Posted on: February 11th, 2024

Serikali wilaya ya  Singida imezitaka shule zote za Msingi na Sekondari kuchukua hatua katika ufundishaji kwa njia ya TEHAMA kwa masomo yenye upungufu wa walimu ikiwa ni moja ya mikakati ya kuinua kiwango cha elimu wilayani humo.

MKuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili ametoa agizo hilo katika kikao kazi cha kupokea taarifa ya hali ya ufundishaji kwa njia ya TEHAMA katika Halmashauri mbili za wilaya Singida ambazo ni Manispaa ya Singida na Halmashauri ya wilaya ya Singida.

Muragili amesema idadi ya shule ambazo zimeanza utekelezaji tangu kutolewa kwa maelekezo ya kufundisha kwa njia ya TEHAMA Oktoba 4, 2023 hairidhishi hivyo kutoa agizo kwa wakurugenzi kuhakikisha kila halmashauri inanunua vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya kufundishia wakati kila shule ikijipanga kununua vifaa vyake.

 

“… wakurugenzi nunueni vifaa hivyo ambavyo kwa sasa vitakuwa vikizunguka kwa kila shule wakati shule zikijipanga kupata vifaa vyao…. Shirikisheni wazazi kupitia vikao na mikutano na wafadhili ili kufanikisha upatikanaji wa vifaa”, amesisitiza.

Jumla ya shule za sekondari 08 na za msingi 13 zimeanza kutekeleza ufundishaji kwa njia ya TEHAMA katika wilaya ya Singida ikiwa shule 6 za sekondari ni za Manispaa ya Singida na 02 kutoka Halmashauri ya wilaya ya Singida. Kwa upande wa shule za msingi Jumla ya shule 11 za Manispaa ya Singida zinafundisha kwa njia ya TEHAMA na shule 02 ni kutoka Halmashauri ya wilaya ya Singida.

Wakiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo lililotolewa mwezi Oktoba 4, 2023 na Mkuu huyo wa wilaya, Maafisa elimu wa Divisheni za elimu Sekondari na Msingi wameeleza changamoto kubwa iliyowakwamisha na kusababisha kusuasua kwa utekelezaji wa agizo hilo ni ukosefu wa vifaa vya TEHAMA

Aidha tayari Idara hizo zimeshaainisha masomo ambayo yanachangamoto ikiwa ni masomo ya hesabu, sayansi na kiingereza kwa shule za msingi wakati kwa shule za sekondari masomo yaliyobainishwa ni kemia, fizikia, baolojia, hesabu na kiingereza.

Pamoja na ubainishaji huo tayari timu za uratibu wa masuala ya ufundishaji kwa njia ya TEHAMA zimeundwa sambamba na kubaini walimu mahiri katika masomo yaliyobainishwa ili kuweza kufanikisha ufundishaji huo.

Akitoa mchango wake Naibu Meya wa Manispaa ya Singida Geophrey Mdama ameunga mkono agizo hilo na kusema ni wakati sasa wa kuamka na kutekeleza kwa vitendo kwani inawezekana kupitia njia shirikishi jamii.

Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Singida Elia Diga amesema agizo limepokelewa na linakwenda kutekelezwa kwa ushirikiano baina ya wataalam, wazazi na wanasiasa kwa maana ya madiwani.

 “Miaka ya 1980 iliwezekana wanafunzi walisoma kupitia redio dararasani kwani sasa tushindwe?” alisisitiza Diga.

Shule zote zimeelekezwa kwenda kuweka mkakati Madhubuti wa kuhakikisha zoezi hilo linatekelezeka kwa mafanikio makubwa.

Wilaya ya Singida ilianza kufufundisha kwa njia ya TEHAMA mapema mwezi Oktoba 2023 kufuatia agizo la Mkuu wa wilaya hiyo Mhandisi Paskasi Muragili ikiwa ni moja ya mikakati ya kuinua kiwango cha elimu wilayani humo.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA AMALI MKOA WA SINGIDA

    May 21, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU PILI

    May 20, 2025
  • MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN ASANTE KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAFANYAKAZI

    May 20, 2025
  • "UPATIKANAJI WA HAKI KUONGEZA IMANI KWA WANANCHI"

    May 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.