• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko/Mrejesho |
Singida Municipal Council
Singida Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Elimu Msingi na Awali
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango, na Uratibu
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
    • Units
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Misitu na Maliasili
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Maziwa
      • Mawe
      • Maeneo ya Kihistoria
    • Kilimo
    • Umeme wa Jua na Upepo
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Usafi wa Mazingira
    • Ukusanyaji wa Mapato
    • Mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu
    • Kituo cha Biashara
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipangomiji,Mazingira, na Ujenzi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Time Table
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/MwenyeKiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyoidhinishwa
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Miongozo ya Kilimo
    • Policy
    • Fomu
    • Taarifa Ya Utekelezaji
    • Jarida
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Sheria
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa Za Kifedha
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WIZARA YA AFYA YAPONGEZA MANISPAA YA SINGIDA KWA USIMAMIZI BORA WA HUDUMA ZA AFYA

Posted on: February 6th, 2025


Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Kinywa na Meno wa Wizara ya Afya, Dkt. Baraka Nzobo, ameipongeza Manispaa ya Singida kwa kazi nzuri inayofanywa katika utoaji wa huduma za afya, akisisitiza kuwa ni muhimu kuendelea kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha huduma bora kwa wananchi.

Dkt. Nzobo aliongoza timu ya wataalam kutoka Wizara ya Afya katika ziara ya usimamizi shirikishi wa miradi na huduma za afya kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida na Kituo cha Afya Sokoine, ambapo timu hiyo ilikagua maeneo mbalimbali yanayotolewa huduma.

 Ziara hiyo ilifanyika , Februari 6, 2025, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Wizara ya Afya kuhakikisha miradi ya huduma za afya inatekelezwa kwa ufanisi katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Timu ya Wizara ya Afya ilikagua maeneo kama vile huduma za wagonjwa wa nje (OPD), huduma kwa mama na mtoto, magonjwa yasiyoambukiza, lishe, huduma za dawa, huduma za utengamavu kwa wazee, ustawi wa jamii, na huduma kwa wateja.

Baada ya ukaguzi, Dkt. Nzobo alitoa pongezi kwa Manispaa ya Singida kwa mafanikio yaliyopatikana, lakini alisisitiza kwamba bado kuna mapungufu machache yanayohitaji kuzingatiwa. Aliwataka watumishi wa hospitali na vituo vya afya kuongeza juhudi katika usimamizi wa mapato, akisema kuwa ukusanyaji wa mapato ni muhimu kwa kuboresha mazingira ya huduma za afya na kuhakikisha hospitali inajitegemea kifedha.

“Ni muhimu kusimamia mapato vizuri, kwani yataisaidia hospitali katika kuendesha huduma na kuboresha mazingira ya hapa. Ikiwa mapato yataendelea kubaki hapa, itakuwa msaada kwa hospitali na watumishi kwa kulipwa stahiki zao bila kutegemea fedha kutoka maeneo mengine,” alisema Dkt. Nzobo.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa kupunguza rufaa zisizo za lazima kutoka hospitali ya Manispaa ya Singida kwenda hospitali za mkoa. “Tunategemea hospitali ya wilaya kuwa na uwezo wa kutoa huduma bora na kumaliza kesi nyingi za wagonjwa hapa, na siyo kuzituma kwenye mikoa mingine,” alisema.

Kuhusu upungufu wa watumishi, Dkt. Nzobo alishauri kuwa Manispaa ya Singida iendelee kufanya juhudi za kuomba vibali kwa ajili ya kuajiri watumishi wa afya ili kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Ziara hii ni sehemu ya juhudi za Wizara ya Afya za kuhakikisha ufanisi wa huduma za afya katika hospitali za wilaya na vituo vya afya nchini.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ March 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO DIRISHA LA ROBO YA TATU January 10, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU MWENYE ULEMAVU KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA October 02, 2024
  • MATOKEO YA VITENDO KWA DEREVA October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari za hivi Punde

  • NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MEI MOSI - MAJALIWA

    April 30, 2025
  • KIKWETE AFUNGA MICHEZO UWANJA WA CCM LITI

    April 30, 2025
  • "UMUHIMU WA MFUMO BORA WA USALAMA WA AFYA KAZINI"

    April 28, 2025
  • "UMUHIMU WA MFUMO BORA WA USALAMA WA AFYA KAZINI"

    April 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOOST HADI TAREHE 02 JUNI 2023 - MANISPAA YA SINGIDA
Video Zaidi

Viunganisho vinavyohusiana

  • Press Release

Kurasa za Karibu

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karume Road Street

    Sanduku la Posta: P.O BOX 236,Singida

    Telephone: +255 26 250 2179/236

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: md.singidamc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Singida.Haki zote zimehifadhiwa.